MAREKANI-DONALD TRUMP

Wajumbe wanaompinga Trump waandamana dhidi ya mkataba wa Republican

Wajumbe wanaompinga Trump wakipuliza filimbi na kupiga kelele,wakipinga uamuzi wa chama cha Republicana kumasisha bilionea huyo kuwania kiti cha urais Marekani Jumatatu, Julai 18, 2016.
Wajumbe wanaompinga Trump wakipuliza filimbi na kupiga kelele,wakipinga uamuzi wa chama cha Republicana kumasisha bilionea huyo kuwania kiti cha urais Marekani Jumatatu, Julai 18, 2016. REUTERS/Mark Kauzlarich

Shughuli za ufunguzi wa mkataba wa chama cha Republican katika mji wa Cleveland zilisambaratishwa Jumatatu Julai 18 na wajumbe wanaompinga Donald Trump. Kwa kisingizio cha kupiga kura ya kiutaratibu, wajumbe hao wamefutilia mbali uamuzi wa chama chao kwa uteuzi wa bilionea huyo kuwania kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo kulikua na maandamano pia dhidi ya kuwania kwa Donald Trump katika uchaguzi wa urais.

Wajumbe wa chama cha Republican walikuwa wakijiandaa kupitisha kanuni ya Mkataba wakati baadhi ya wajumbe miongoni mwao wanaompinga Donald Trump, walionyesha kutoridhika kwao. Wakidai kufanyika kwa uchaguzi, iwakati ambapo utaratibu wa kumpitisha Donald Trump bila kupigiwa kura ulikua ukitazamiwa kufanyika, baadhi ya wajumbe wanaompinga bilionea huyo walipiga kelele na kupuliza filimbi dhidi ya viongozi wengine wa chama cha Republican. "Kura! " alilalamika mjumbe mmoja kutoka jimbo la Virginia, huku akisimama juu ya kiti na wajumbe wengine waliopinga wakitaka kura ipigwe ili kuweka takwimu juu ya mfarakano wa chama.

Lakini rais wa kikao amepuuzia jambo hilo, kwa kupitisha uamuzi wa wa chama bila ridhaa ya baadhi ya wajumbe. Kulikua na mvutano mkali kati ya wajumbe wanaomuunga mkono Trump na wale wanaompinga. Licha ya hali hiyo kila upande ulipiga kura na hivyo mvutano kumalizika.

Maandamano dhidi ya sera zilizopewa kipaombele na Donald Trump

Katika mji wa Cleveland, raia wanaompinga Donald Trump pia waliingia mitaani. Hata kabla ya kuanza kwa makubaliano hayo, mikutano ya kulaani sera zilizopewa kipaombele na mgombea wa Ikulu ya White House ilikuwa tayari kupangwa katikati ya jiji. CAIR, Jumuiya ya Kiislamu na inayopambana kwa ajili ya haki za kiraia, iliwakusanyika watu zaidi ya watu mia moja kwa kulaanisera dhidi ya jamii yao.

Ahmed, Imam wa msikitimmoja katika eneo la Akron, katika mji wa jimbo la Ohio karibu na mji wa Cleveland, alikuwa miongoni mwa waandamanaji. "Kwa kuwa mtu wa busara, wakati nilisikia kwa mara ya kwanza, nilifikiri ni utani. Alizungumza ujinga. Na kauli yake ilituumiza sanai. Kilichonisikitisha ni kwamba aliungwa mkono na watu wengi. Wananchi wenzangu wanaunga mkono sera kama hizo. Sera zilizojaa sumu na ambazp zinachochea chuki na mgawanyiko. Sera ambazo haziwezi kukubalika katika jamii inayounda na watu kutoka tabaka mbalimbali, " Ahmed ameiambia RFI.