MAREKANI-DONALD TRUMP

Trump ateuliwa rasmi kuwa mgombea wa chama cha Republican

Baada ya uteuzi wake katika mkataba wa chama cha Republican mjini Cleveland, Donald Trump alizungumza kupitia satellite video kutoka mjini New York, Julai 19, 2016.
Baada ya uteuzi wake katika mkataba wa chama cha Republican mjini Cleveland, Donald Trump alizungumza kupitia satellite video kutoka mjini New York, Julai 19, 2016. REUTERS/Mike Segar

Donald Trump ameapishwa kama mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais nchini Marekani katika rais siku ya pili ya kusanyiko la Chama cha Conservative Jumanne Julai 19. Uchaguzi, uliokua umepangwa kufanyika Jumatano hii, umefupizwa na kufanyika jana Jumanne, bila kujua sababu.

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump atakua mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi ujao wa rais wa mwezi Novemba. Bilionea huyo ameteuliwa rasmi Jumanne hii usiku katika mji wa Cleveland na wajumbe wa chama cha Republican ili kujaribu kumuangusha Hillary Clinton na kumrithi Barack Obama.

Ikilinganishwa na matokeo ya kura za mchujo, Donald Trump, mwenye umri wa miaka amepata ushindi mkubwa, kwa kura za wajumbe 1,725 waliompigia kura kwa jumla ya wajumbe 2472 walioshiriki zoezi hili.

Ni mwanawe Donald Jr aliyetangaza kuungwa mkono kwa wajumbe 89 kutoka katika jimbo la New York ambapo anazaliwa bilionea huyoUungwaji mkono huyo ulipelekea idadi ya wajumbe inayohitajika kuvuka kiasi na kupata ushindi mkubwa. "Hongera Baba, tunakupenda," mawanawe amesema, huku akizungukwa na ndugu na dada zake.

Baaadhi ya wajumbe vigogo wa chama cha Republican waalijaribu kwa mara nyingine mara ya mwisho kuzuia uteuzi wake, lakini jaribio la kubadili sheria ya Mkataba lilishindwa Jumatatu.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Paul Ryan, akitangaza Donald Trump mshindi wa kura za mchujo katika chama cha Republican, Jumanne, Julai 19, 2016.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Paul Ryan, akitangaza Donald Trump mshindi wa kura za mchujo katika chama cha Republican, Jumanne, Julai 19, 2016. REUTERS/Carlo Allegri