Brazil: Watu 10 wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa IS wakamatwa

Serikali ya Brazil imetangaza kwamba kumekuwa na kundi la kigaidi ambalo limekuwa likiandaa mashambulizi wakati wa michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro.

Wanajeshi na askari polisi 85 000watatumwa katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha usalama wa Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro, Brazil.
Wanajeshi na askari polisi 85 000watatumwa katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha usalama wa Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro, Brazil. REUTERS/Bruno Kelly
Matangazo ya kibiashara

Alhamisi hii Julai 21, polisi ya Brazil imesema imewakamata vijana 10 wanaotuhumiwa kupanga mashambulizi wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro. Siku ya Jumatatu, wafuasi wa Brazil wa kundi la Islamic State waliaminika kuingia nchini humo.

Wakati ambapo Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro inatazamiwa kuanza Agosti 5, polisi ya Brazil imetangaza Alhamisi hii kuwakamata vijana 10 wanaotuhumiwa kupanga mashambulizi wakati wa Michezo ya Olimpiki. Wote ni Wabrazil, na mmoja wao ni mdogo, amesema Waziri wa Sheria, Alexandre de Moraes, akiwaambia waandishi wa habari mjini Brasilia. Baadhi ya vijana hao walikula kiapo kutii nadharia ya kundi la Islamic State "kupitia mtandao" na walijaribu kununua bunduki,Waziri wa Sheria wa Brazil amebaini. "Walikua wakiwasiliana kupitia Whatsapp na Telegram na wawili wamelijuana kabla. Kiongozi wao ni kutoka jimbo la Parana (kusini), "ameongeza Waziri.

Kuibuka kwa kundi la wanajihadi kutoka Brazil?

Watuhumiwa hawo kumi walikua wakifuatiliwa tangu mwezi Aprili, na "walikua wakishiriki katika kundi liitwalo "watetezi wa Sharia" na walikua wamepanga kupata silaha kwa lengo la kufanya uhalifu nchini Brazil na hata nje ya nchi," amesema Waziri Alexandre Moraes. Katika taarifa yake, Wizara ya Sheria inasema kwamba "polisi ya Brazil ilizingua Alhamisi hii operesheni inayoitwa Hashtag, ili kuliangamiza kundi lililoshiriki kuendelea kundi la Islamic State nchini Brazil na katika utekelezaji wa vitndo vya maandalizi kwa ajili ya ukuendesja mashambulizi ya kigaidi na vitendo vingine vya uhalifu. "