SIASA-MAREKANI

Mwenyekiti wa chama cha Democratic nchini Marekani kujiuzulu

Debbie Wasserman Schultz Mwenyekiti wa chama cha Democratic nchini Marekani
Debbie Wasserman Schultz Mwenyekiti wa chama cha Democratic nchini Marekani Washtimes

Mwenyekiti wa chama cha Democratic nchini Marekani Debbie Wasserman Schultz ametangaza kuwa atajiuzulu wadhifa huo, baada ya kuvuja kwa taarifa za kutaka umoja ndani ya chama hicho wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho unaoanza hivi leo katika mji wa Philadelphia.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya kuwepo kwa madai kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho walijaribu kuzuia kuendelea kwa kampeni za Bwana Bernie Sanders aliyekuwa anapambana na Hillary Clinton kutafuta tiketi ya chama hicho.

Sanders ambaye alitangaza kumuunga mkono Bi.Clinton katika dakika za lala salama amekuwa akishinikiza kujiuzulu kwa mwenyekiti huyo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.

Wajumbe wa chama hicho wanatarajiwa kumpitisha Bi. Clinton kupeperusha bendera ya chama hicho wakati wa uchaguzi wa urais mwezi Novema mwaka huu atakapopambana na Donald Trump wa chama cha Republican.

Hillary Clinton kushoto akiwa na mgombea mweza wake Tim Kaine
Hillary Clinton kushoto akiwa na mgombea mweza wake Tim Kaine SAUL LOEB / AFP

Bi.Clinton alimteau Tim Kaine kuwa mgombea mwenza wake.

Rais Barrack Obama, mkewe Mitchel na Bernier Sanders ni miongoni mwa watu watakaozungumza katika mkutano huo wa siku mbili.