MAREKANI-URUSI

Kremlin yakanusha madai ya kumpigia debe Trump

Donald Trump, kati ya mtoto wake Eric (kulia) na meneja wa kampeni zake Corey Lewandowski (kushoto) wakikaribisha matokeo ya kura za mchujo katika majimbo ya Florida, Ohio, North Carolina, Illinois na Missouri (Palm Beach Machi 15, 2016).
Donald Trump, kati ya mtoto wake Eric (kulia) na meneja wa kampeni zake Corey Lewandowski (kushoto) wakikaribisha matokeo ya kura za mchujo katika majimbo ya Florida, Ohio, North Carolina, Illinois na Missouri (Palm Beach Machi 15, 2016). REUTERS/Joe Skipper

Ikulu ya Kremlin, Jumatano hii, imekanusha suala la kuingilia katika kampeni za uchaguzi wa Marekani baada ya kauli ya Rais Barack Obama kuwa Urusi huenda inatafuta kumpigia debe mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump, ili aweze kushinda mbio za kuwania urais nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Ndani ya siku kadhaa, hali ya vita baridi inayoyakumba mahusiano ya miaka miwili kati ya Washington imeingizwa katiika kampeni za uchaguzi wa urais nchini Marekani.

Sababu? Kuvuja kwa barua pepe za maafisa wandamizi wa chama cha Democratic, zilizowekwa hadharani na tovuti ya Wikileaks siku moja kabla ya ufunguzi wa mkutano wa chama cha Democratic na ambazo zilionyesha dharau ya viongozi wa chama kwa Bernie Sanders, mshindani wa zamani wa Hillary Clinton katika kura za mchujo za chama cha Democratic. Bila kuchelewa, viongozi wa chama cha Democratic na wataalam wa masuala ya udukuzi waliinyooshea kidole cha lawama Urusi na washirika wake na kuituhumu Ikulu ya Kremlin kutafuta kumdhoofisha Clinton kumtukuza Donald Trump.

Jumatano hii ilikuwa ni zamu ya Barack Obama kubainisha, kwa uhakika mchango wa Urusi kwa tuhuma hizo: "Kila kitu kinawezekana," amesema Barack Obama, akihojiwa na kituo cha habari cha televisheni cha NBC, kuhusu uwezekano wa Urusi katika kesi hii.

"Tunachokijua ni kwamba Urusi imekua ikifanya udukuzi wa mifumo yetu. Si tu ile ya serikali, lakini pia mifumo binafsi," Obama ameongeza.

Lakini mbali na udukuzi, ni suala la upendeleo analotuhumiwa Vladimir Putin kwa Donald Trump kama rais wa Marekani aliamuru katika mjadala.

"Nadhani Trump amepopata msaada mzuri kutokakwa Urusi," amesema Bw Obama, kabla kukumbusha kwamba Donald Trump "alionyesha mara kadhaa jinsi gani anavyoshikamana na Vladimir Putin."

"Sina uhusiano wowote na Urusi, " amejitetea kwa upande wake Jumatano hii Donald Trump mbele ya vyombo vya habari, akisisitiza kuwa hajawahi kukutana na rais wa Urusi.

Kwa upande wake, Ikulu ya Kremlin, imejibu kupitia msemaji wake Dmitry Peskov : "Rais Putin amerejea mara kadhaa kwamba Urusi, kamwe, haijawahi kuingilia na haingilia masuala ya ndani (ya nchi), hasa katika mchakato wa uchaguzi wa nchi nyingine. "