MEXICO-MAFURIKO

Watu zaidi ya 40 wapoteza maisha kufuatia maporomoko ya udongo

Katika baadhi ya majimbo ya Mexico, majumba yameshambuliwa na maporomoko ya matope kama hapa Morro dos Prazeres katika jimbo la Santa Tereza, karibu na katikati mwa mji wa Rio.
Katika baadhi ya majimbo ya Mexico, majumba yameshambuliwa na maporomoko ya matope kama hapa Morro dos Prazeres katika jimbo la Santa Tereza, karibu na katikati mwa mji wa Rio. Reuters / Bruno Domingos

Katika baadhi ya mikoa nchini Mexico, mvua kubwa zimekua zikinyesha kwa muda wa masaa 24 "jumla ya kiwango cha mvua zinazonyesha kwa mwezi mzima." Kwa uchache watu 40 wamepoteza maisha kufuatia maporomoko ya udongo kutokana na mvua hizo.

Matangazo ya kibiashara

Hali hii inashuhudiwa katika majimbo ya Puebla (katikati) na Veracruz (mashariki), kutokana na maporomoko ya udongo yanayosababishwa na dhoruba iitwayo Earl. Dhoruba mpya inatarajiwa kupiga katika masaa machache yajayo katika pwani ya Pasifiki ya Mexico, mamlaka ya hali ya hewa nchini Mexico imebaini.

Taarifa iliyotolewa Jumapili na serikali ya jimbo la Puebla, watu 29, wakiwemo watoto 15, walipoteza maisha wakati nyumba zao zilivamiwa na maporomoko ya udongo. Katika jimbo la Veracruz, watu kumi na mmoja walipoteza maisha katika hali kama hiyo, kwa mujibu wa mkuu wa jimbo hilo.

Tishio la dhoruba mpya

Mkuu wa wa Jimbo la Puebla, Rafael Moreno Valle amezuru mji wa Huauchinango kutathmini uharibifu uliyosababishwa na dhoruba hiyo na kuratibu misaada. "Hatutopumzika mpaka hali hii ishughulikiwe," amesema Rafael Moreno, katika ujumbe kwenye akaunti yake Twitter, huku akiweka picha za maeneo yaliyoathirika zaidi na kimbunga hicho, ambapo moja inaonyesha jinsi nyumba ilivyoshambuliwa kwa mafuriko ya matope.