MAREKANI-GUANTANAMO-UGAIDI

Guantanamo: wafungwa kumi na tano wahamishiwa UAE

Raia wa Yemen kumi na wawili na watatu kutoka Afghanistan watahamishwa kutoka Guantanamo kwenda Umoja Falme za Kiarabu (UAE).
Raia wa Yemen kumi na wawili na watatu kutoka Afghanistan watahamishwa kutoka Guantanamo kwenda Umoja Falme za Kiarabu (UAE). REUTERS/Bob Strong

Nchini Marekani, Pentagon ilitangaza Jumatatu hii kufanyika kwa zoezi la kuwahamisha wafungwa wa 15 kutoka jela la Guantanamo kwenda Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Hili ni zoezi kubwa tangu kuwasili kwa Barack Obama katika Ikulu ya White House nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani aliahidi mwaka 2009 kwamba atalifunga jela la Guantanamo lililojengwa kwenye mpaka wa Marekani na Cuba, baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001 katika mji wa New York, lakini inaonekana hatoweza kutimiza ahadi yake kabla ya mwisho wa mwaka huu, ambapo atakua amekamilisha mihula yake miwili na kuondoka madarakani. Baada ya kabiliwa na ugumu wa kupata maeneo, nchini Marekani au mahali pengine, kwa ajili ya kuwahifadhi wafungwa, Washington imeishukuru Abu Dhabi.

Raia kumi na wawili kutoka Yemen, ambao hawawezi kutumwa nchini mwao ambayo inakumbwa na vita, na raia watatu kutoka Afghanistan, ni miongoni mwa wafungwa kumi na tano watakaohamishiwa katika Umoja wa Falme za Kirabu. Serikali ya Abu Dhabi sasa itawajibika kwa ajili yao: kwa ujumla, wafungwa hawa wa Guantanamo wameachiwa huru chini ya masharti ya utaratibu wa usimamizi na ufuatiliaji wa kuwaunganisha na mpango wa kuwakutanisha na familia zao.

Marekani imekaribisha Umoja wa Falme za Kiarabu kwa "kukubali kuwapokea wafungwa hao" na "nia ya kusaidia juhudi inayoendelea kwa kufunga jela la Guantanamo." "Vita dhidi ya ugaidi" vilipelekea jea hilo kujaa haraka; watu 780 ikiwa ni pamoja na wasio na hatia wamekua wakizuiliwa katika jela hilo.

Wafungwa hamsini bado kuhamishwa

Lakini Marekanisasa inajitahidi kuifunga jela la Guantanamo. Walikua wafungwa 242 wakati Barack Obama alchukua hatamu ya uongozi wa nchi, na licha ya wafungwa kuachiliwa huru kwa mfululizo katika miezi ya hivi karibuni, bado kunasalia wafungwa 61 katika jela la Guantanamo, na kati yao, baadhi yao, wafungwa hamsini hawatahamishwa na wala hawawezi kuhukumiwa na mahakama ya kawaida.