Mexico: Watu zaidi ya 10 watekwa nyara katika mgahawa wa La Leche

Gari lililoharibiwa wakati wa operesheni ya kijeshi ya kujaribu kukamata kundi la El Chapo linalifanya biashara haramu ya madawa ya kulevya tarehe 18 Oktoba katika Jimbo la Durango,  kaskazini-magharibi mwa Mexico.
Gari lililoharibiwa wakati wa operesheni ya kijeshi ya kujaribu kukamata kundi la El Chapo linalifanya biashara haramu ya madawa ya kulevya tarehe 18 Oktoba katika Jimbo la Durango, kaskazini-magharibi mwa Mexico. AFP PHOTO/RONALDO SCHEMIDT

Watu wenye silaha wamewateka nyara watu wasiopungua 10 Jumatatu hii katika mgahawa wa La Leche katika eneo la mapumziko la Puerto Vallarta nchini Mexico , katika jmbo la Jalisco (magharibi). Inawezekana kuwa huenda tukio hilo ni la upizaji kisasi kati ya makundi hasimu, viongozi wa jimbo hili wamsema.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la watu wenye silaha walivamia alfajiri mgahawa wa La Leche, unaopatikana katika eneo hilo la mapumziko, karibu na hoteli kadhaa za kimataifa.

Kati ya watu "10 na 12" walitekwa nyara, kwa mujibu wa Mwendesha mashitaka katika jimbo laJalisco, Eduardo Almaguer.

"Kuna dalili kali kuwa watu hao walikuwa katika kundi la uhalifu. Haikuwa watalii au wananchi wanaoendesha shughuli halali," Eduardo Almaguer amewaambia waandishi wa habari.

"Tunaamini kwamba watekaji nyara ni kutoka kundi hasimu," ameongeza Bw Almaguer.

Kwa mujibu wa Mwendesha mashitaka, magari manne ya kifahari ya watu hao waliotekwa nyara yalitelekezwa karibu na mgahawa. Angalau moja ya magari hayo yalikuwa yametangazwa kwa udanganyifu.

Eneo la Puerto Vallarta, ambalo linapatikana katika pwani ya Pasifiki ya Mexico, liko katika eneo linalodhibitiwa na kundi la wapiganaji la Jalisco New Generation lililoanzishwa mwaka 2010 baada ya kifo cha Ignacio "Nacho" Coronel, kiongozi wa kundi la Sinaloa.

Katika miaka ya hivi karibuni, kundi la Jalisco New Generation liimekuwa moja ya makundi yanayofanya biashara haramu ya madawa ya kulevya nchini Mexico, likiwa na mitandao katika bara la Asia au Ulaya.Mwaka 2015 kundi hili liliiangusha helikopta ya jeshi kwa kutumia silaha ya kurusha kombora na kusababisha vifo vya askari saba.