MAREKANI-TRUMP

Trump aweka wazi mkakati wake wa kupambana na ugaidi

Mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump.
Mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump. REUTERS/Eric Thayer

Donald Trump ameelezea mkakati wake wa kuifanya Marekani ina kuwa salama hasa dhidi ya dhidi ya vitendo vya kigaidi vinavyotekelezwa na Waislamu wenye msimamo mkali wa itikadi za kigaidi. "Nina wapinzani wengi, lakini adui wangu ni mmoja, "Msimamo mkali wa itikadi za Kiislam za kigaidi," amesema Trump

Matangazo ya kibiashara

Kundi la Islamic State (IS) ni miongoni mwa makundi yanayolengwa na Donald trump ili Marekani iwe na usalama wa kudumu. Mgombea urais wa chama cha Republican ameitaja pia Iran, kama "mdhamini wa kwanza" wa ugaid huo, kundi la al-Qaida, ambalo anatarajia "kuliangamiza" kundi la Hezbollah kutoka Lebanon na chama cha Hamas nchini Palestina, bila kusahau maeneo yote duniani yaliyoambukizwa uovu huo au uhalifu huo na wahusika wao.

Wakati wa hotuba ya Jumatatu katika jimbo la Ohio, Donald Trump, ambaye alikabiliwa na hali ya sintofahamu kwa wiki kadhaa, amesema ana imani kwamba raia wa Marekani kwa ujumla wanatarajia uchaguzi wa urais ili kufafanua sera yake ya kigeni iwapo atachaguliwa Novemba 8 kuwa rais wa Marekani. Ameelezea pia juu ya umuhimu wa mpango wa muda wa kuzuia viza za waombaji wanaotoka katika nchi ambazo zina historia ya kueneza ugaidi ,na kupendekeza kuanzishwa kwa mifumo ya uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa akauti zao za mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa Trump, juhudi zote lazima sasa ziwekwe pamoja kwa lengo moja, kuliangamiza kundi la Daech (IS), wauaji wake na itikadi yake. Hii inahitaji vipengele vkuu viwili: kujua wale wanaoshirikiana na kundi hili na kuimarisha bila shaka sera ya uhamiaji.

Bwana Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na nchi yoyote ile bila kujali tofauti za kiitikadi au mikakati akiwa na nia ya kusaidia kulitokomeza kundi la Islamic State.

"Nchi yoyote ambayo itachangia kwa lengo letu itakuwa mshirika wetu, ameonya mgombea wa chama cha Republican. Hatuwezi daima kuchagua marafiki zetu, lakini hatupaswi kamwe kushindwa kutambua maadui zetu. " Trump ametaja kama sehemu ya kambi sahihi: Mfalme Abdullah wa Jordan, Abdel Fatah Al-Sissi wa Misri na Vladimir Putin nchini Urusi, ambaye "tunaweza kupata sehemu ya maelewano kwa kupambana na ugaidi", amesema Donald Trump.