COLOMBIA-FARC

Serikali ya Colombia na waasi wa FARC wasaini mkataba wa amani wa kihistoria

Ivan Marquez, kiongozi wa ujumbe wa waasi wa FARC katika mazungumzo (kushoto) akimshika mkonoHumberto de la Calle (kulia), wakati wa mkataba wa amani kihistoria uliotiliwa saini katika mji wa Havana, Agosti 24, 2016.
Ivan Marquez, kiongozi wa ujumbe wa waasi wa FARC katika mazungumzo (kushoto) akimshika mkonoHumberto de la Calle (kulia), wakati wa mkataba wa amani kihistoria uliotiliwa saini katika mji wa Havana, Agosti 24, 2016. REUTERS/Alexandre Meneghini

Serikali ya Colombia na waasi wa FARC walitangaza Jumatano wiki hii katika mji wa Cuba kuwa waliafikiana kutiana saini mkataba wa amani wa kihistoria baada ya karibu miaka minne ya mazungumzo yenye leno la kukomesha vita viliyodumu miaka 52.

Matangazo ya kibiashara

"Tumefikia makubaliano ya mwisho, kamili na ya kudumu kuhusu masuala yote yaliyokua katika ajenda" ya mazungumzo yaliyofanywa tangu mwezi Novemba 2012 katika mji wa Havana, kulingana na waraka uliyotiliwa saini na pande zote mbili na kusomwa na mwanadiplomasia wa Cuba Rodolfo Benitez, ambapo nchi yake pamoja na Norway zilifutilia kwa karibu mazungumzo hayo.

"Makubaliano haya ya mwisho kwa lengo la kumaliza mgogoro uliyokua ukiendelea na kujenga amani imara na ya kudumu hatimaye yatakomesha viliyodumu zaidi ya miaka 50," imeongeza nakala ambayo imezungumzia kwa ufupii pointi kuu za mkataba.

"Sasa tunaweza kutangaza kwamba mapigano yamemalizika, na kuanza mapambano ya mawazo, mkataba huu ni hatua ya mwanzo, sio mwisho," amesema muda mfupi baada ya tangazo hili kiongozi wa ujumbe wa waasi wa FARC katika mazungumzo hayo, Ivan Marquez, akibaini mabadiliko ya baadaye ya kundi hilo la waasi kuwa chama cha kisiasa.

Akiwa mjini Bogota, Rais wa Colombia Juan Manuel Santos amekaribisha kwa furaha kubwa" kuafikiwa kwa lmkataba wa amani na kukaribisha mwisho wa vita.