UN-ANTONIO GUTERRES

UNSC yamteua rasmi Antonio Guterres kuwa Katibu Mkuu wa UN

Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno Antonio Guterres akiongea kutoka Lisbon, Alhamisi, Oktoba 6, 2016.
Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno Antonio Guterres akiongea kutoka Lisbon, Alhamisi, Oktoba 6, 2016. REUTERS/Rafael Marchante

Raia huyu wa Ureno amepata uungwaji mkono wa wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kumrithi Ban Ki-moon kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Bw Guterres anatazamiwa kupitishwa na kamati kuu, na hatua hii itakua ya mwisho, kabla ya kuchukua mamlaka ya Uongozi Januari 1 mwakani.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno ameteuliwa Alhamisi wiki hii kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa baada ya kuongoza kwa miaka kumi shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi UNHCR.

Jina lake limepitishwa kwa kauli moja. Antonio Guterres amepata uungwaji mkono wa wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na atakua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwa mujibu wa wanadiplomasia baada ya mkutano wa faragha. Waziri mkuu wa zamani wa Ureno alikua alipewa nafasi kubwa ya kushinda kwenye nafasi hiyo baada ya kuongoza katika kura sita za awali. Mapendekezo ya wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yatawasilishwa katika kamati kuu ya baraza hilo, yenye wajibu wa kumchagua Katibu Mkuu.

Antonio Guterres atakua mtu wa tisa kushikilia nafasi hii muhimui tangu kuundwa kwa Umoja wa Mataifa mwaka 1945. Atamrithi raia kutoka Korea Kusini Ban Ki-moon, ambaye muhula wake wa pili wa miaka mitano unamalizika mwishoni mwa mwaka huu. "Namjua vizuri, Antonio Guterres, na ninamchukulia kuwa ni chaguo bora" Katibu Mkuu wa sasa wa Umoja wa Mataifa amekaribisha. "Uzoefu wake kama zamani Mkuu wa Ureno, elimu yake kubwa ya mambo ya dunia na akili yake ni muhimu sana kwa kuongoza Umoja wa Mataifa wakati huo muhimu."

• Miaka kumi katika uongozi wa UNHCR

Antonio Guterres, mwenye umri wa miaka 67, aliliongoza shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) tangu mwaka 2005 hadi mwaka 2015 kama Kamishna Mkuu wa shirika hilo.

Antonio Guterres atakuwa katibu mkuu wa kwanza wa umoja wa Mataifa ambaye alikuwa kiongozi wa juu kwenye Serikali ya nchi yake, nafasi ambayo mara nyingi ilikuwa inakaliwa na mawaziri wa mambo ya nje.

Kulikuwa na wagombea 10 kwenye mbio hizo za kuwania ukatibu mkuu wa umoja wa Mataifa, akiwemo waziri wa mipango wa umoja wa Ulaya, Kristalina Georgieva kutoka Bulgaria ambaye aliingia kwenye mbio hizo juma lililopita.

Makamu wa rais wa zamani wa benki ya dunia, Georgieva alishindwa kupata uungwaji mkono kutoka kwa nchi 2 wanachama wa kudumu wa baraza la usalama, huku kukiwa na taarifa za ndani kuwa, Urusi ilimpinga.

Mkuu wa shirika la UNESCO Irina Bokova, ambaye alitengwa na Serikali ya Bulgaria akitakiwa kumpisha Georgieva alipata kura mbili hasi kutoka kwa nchi tano zenye kura za turufu.