MAREKANI-CLINTON-TRUMP

Trump asema hatajiondoa katika kinyang’anyiro cha uraisi

Mgombea uraisi nchini Marekani kupitia chama cha Republican
Mgombea uraisi nchini Marekani kupitia chama cha Republican 路透社

Mgombea uraisi nchini Marekani kupitia chama Republican Donald Trump amesema hatojiondoa katika mbio za kuelekea ikulu na kuwaangusha wafuasi wake.

Matangazo ya kibiashara

Shinikizo kubwa limeibuka juu yake kufuatia kanda ya video ya mwaka 2005 ambayo anaonekana akitoa maneno machafu kuhusu wanawake anasikika akijigamba kuhusu kuwagusa wanawake sehemu zao za siri na kujaribu kushiriki ngono nao.

Trump ameliambia jarida moja nchini Marekani kuwa hakuna nafasi ya kujiondoa katika kinyang’anyiro cha uraisi kwa kuwa anao uungwaji mkono.

Kufuatia video hiyo Trump ameomba radhi na kusema maneno hayo siyo taswira ya vile alivyo.

Maafisa wakuu wa chama cha Republican ambao wameshutumu vikali matamshi yake akiwemo spika wa bunge, Paul Ryan wanasema hawawezi ruhusu Trumph kuwa raisi wa Marekani.