Mjadala wa Wiki

Kampeni nchini Marekani zaingia katika kipindi cha lala salama

Sauti 13:37
Donald Trump na  Hillary Clinton, wagombea urais nchini Marekani
Donald Trump na Hillary Clinton, wagombea urais nchini Marekani REUTERS/Carlos Barria

Kampeni za urais nchini Marekani zinafikia mwisho, kuelekea uchaguzi wa urais wiki ijayo. Ushindani ni kati ya Hillary Clinton wa chama cha Democratic na Donald Trump wa chama cha Republican. Wiki moja kuelekea siku ya kupiga kura, mgombea wa Democratic Bi.Clinton amekabiliwa na sakata la kuchunguza upya barua pepe zilizofutwa wakati akiwa Waziri wa Mambo ya nje. Nani atashinda Uchaguzi huu ? Tunajadili.