ICC-MAREKANI-AFGHANISTAN

ICC: Majeshi ya Marekani nchini Afghanistan huenda yametenda makosa ya kivita

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya ICC, Fatou Bensouda, 14 November 2013 .
Mwendesha mashtaka wa mahakama ya ICC, Fatou Bensouda, 14 November 2013 . UN Photo/Eskinder Debebe

Mwendesha mashtaka mkuu kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, amesema kuwa, huenda wanajeshi wa Marekani walioko nchini Afghanistan, wametenda makosa ya kivita kati ya mwaka 2003 na 2004. 

Matangazo ya kibiashara

ICC inasema kuwa makosa hayo ni pamoja na kuteswa kwa wafungwa, sera ambayo inaonekana ni ya kukusudiwa iliyoidhinishwa na utawala wa washington.

Akitoa matokeo ya uchunguzi wa awali uliofanywa kuhusu uhalifu dhidi ya binadamu nchini Afghanistan, mwendesha mashataka mkuu wa mahakama hiyo, Fatou Bensouda, amesema ataamua ikiwa aombe kufunguliwa kwa jalada kamili la uchunguzi na kuwachukulia hatua wahusika wa vitendo hivyo kwa kuwafikisha mbele ya mahakama hiyo.

Kundi la Taliban linadhibiti kwa sasa kati ya 20% na 35%  ya nchi ya Afghanistan.
Kundi la Taliban linadhibiti kwa sasa kati ya 20% na 35% ya nchi ya Afghanistan. AFP PHOTO / Noorullah Shirzada

Bensouda amesisitiza kuwa, wapiganaji wa Taliban na makundi mengine yenye uhusiano nao kama mtandao wa Haqqani, vikosi vya Serikali vya Afghanistan na vikosi vya Marekani pamoja na shirika la ujasusi la CIA, wote wameonekena kutekeleza makosa ya kivita toka wapiganaji hao wa kiislamu walipofurushwa nchini humo na muungano wa majeshi ya Marekani mwaka 2001.

Mwendesha mashtaka huyo pia, amewalaumu wapiganaji wa Taliban na washirika wake kwa kuhusika na mauaji ya raia elfu 17 toka mwaka 2007 hadi Decemba 2015, katika vita mbaya zaidi kuendeshwa na kundi hilo linalotekeleza mashambulizi kulenga shule, hospitali na misikiti.

Hata hivyo kwa mara ya kwanza, Bensouda ameainisha tuhuma za makosa ya kivita na mateso dhidi ya raia, kulikotekelezwa na majeshi ya Marekani yaliyopelekwa nchini Afghanistan, ambapo yalianzisha vituo vya siri vilivyokuwa vikiendeshwa na majasusi wa CIA wa Marekani.

Wanajeshi wa Afghanistan wakiwa kwenye doria.
Wanajeshi wa Afghanistan wakiwa kwenye doria. REUTERS/Omar Sobhani

Kulikuwa na "ushahidi wa kutosha kuamini kuwa" wakati watuhumiwa wakihojiwa na wanajeshi wa Marekani na majasusi wa CIA, matokeo yake yaliishia kwa watuhumiwa hao kuteswa na hata kubakwa.

Ugumu wa uchunguzi anaotaka:

Ikiwa mwendesha mashataka mkuu Fatou Bensouda ataomba majaji wa mahakama hiyo kuruhusu kufunguliwa kwa uchunguzi kamili wa makosa yaliyotekelezwa nchini Afghanistan, ofisi yake itakuwa inachukua kesi ngumu na ya kisiasa kuwahi kuchunguzwa hivi karibuni.

Wanajeshi wa Afghanistan wakiwa na wanajeshi wa Marekani mjini Kabul
Wanajeshi wa Afghanistan wakiwa na wanajeshi wa Marekani mjini Kabul REUTERS/Omar Sobhani

Kwa upande mwingine pia, nchi ya Marekani yenyewe haijatia saini mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama hiyo, na ni wazi kuwa uwezekano ni mdogo sana kwa utawala wa Washington kutoa ushirikiano wa kutosha kwa uchunguzi wowote utakaolichafua jeshi la nchi yake kwa mara ya kwanza, kuchunguzwa na ICC.

Na hata wakati huu Serikali ya Marekani ikiwa mstari wa mbele kushinikiza wahusika wa mzozo wa Syria kufikishwa kwenye mahakama hiyo kwa makosa ya kivita, nafasi ni finyu sana kwa wanajeshi wake kuishia kwenye mikono ya ICC.