COLOMBIA-FARC

Colombia: mkataba mpya kusainiwa Alhamisi hii

Le président colombien Juan Manuel Santos lors d'une allocution à Bogota, le 22 novembre 2016.
Le président colombien Juan Manuel Santos lors d'une allocution à Bogota, le 22 novembre 2016. Colombian Presidency /Handout via Reuters

Mkataba wa amani kati ya serikali ya Colombia na kundi la waasi wa FARC utasainiwa leo Alhamisi, Novemba 24 saa 11 jioni saa za Colombia katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bogota.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya nakala ya mkataba wa amani uliosainiwa Septemba 26, 2016 kukataliwa kwa kura ya maoni, serikali na upinzani walizidisha mikutano yao. Na Rais Juan Manuel Santos aliamua kuongeza kasi kwa utaratibu huo.

Rais Juan Manuel Santos anaamini kwamba muda wa usitishwaji wa mapigano ulioongezwa hadi mwisho wa mwaka huu bado ni tatizo. Matukio kadhaa yalitokea katika siku za karibuni. Viongozi kadhaa wa kijamii waliuawa katika wiki za hivi karibuni. waasi wana hofu yakutokea mauaji dhidi yao kama yale yaliyotokea mapem amwaka 1990, wakati zaidi ya wanaharakati 3000 wa wa chama cha mrengo wa kushoto cha Patriotic Union, waliuawa.

Kwa muda wa wiki kadhaa, waasi walianza kukusanyika katika maeneo waliotengewa makambi, kwa lengo la kurejeshwa katika maisha ya kiraia. Lakini kutokana na kura ya "hapana" iliyoshinda katika kura ya maoni, kila kitu kilisimamima. Viongozi kundi la waasi la FARC watawaeka wapiganaji wao katika maeneo maalumu wakati ambapo ulinzi ulioafikiwa latika mikataba haujatekelezwa.

Rasimu mpya ya mkataba wa amani, itawasilishwa kwenye baraza la Congress kwa ajili ya kuidhinishwa, ambapo sasa Serikali imekwepa kufanya kura nyingine ya maoni, imesema taarifa ta wapatanishi wa mzozo huo.

Mwezi uliopita, wananchi walioshiriki kwenye kura ya maoni, waliukataa mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya Serikali na waasi wa FARC, wadadisi wa mambo wakisema kuwa, waasi walionewa huruma sana, wakati wametekeleza makosa ya uhalifu wa kivita.

"Serikali na wajumbe wa kundi la FARC wamekubaliana kutia saini makubaliano ya mwisho ili kumaliza mzozo uliodumu kwa miongo kadhaa na kuijenga nchi hiyo upya kupitia maridhiano," wamesema wapatanishi kutoka pande zote mbili.

Mkataba mpya wa amani ulitangazwa kwa mara ya kwanza mwezi Novemba 12 na sherehe za utiaji saini zitafanyika mjini Bogota, Alhamisi ya wiki hii.

Mkataba huu sasa utawasilishwa kwa baraza la Congress kwaajili ya kupigiwa kuwa, mkataba ambao sasa huenda ukapitishwa hasa kutokana na ukweli kuwa, baraza la Congress lina wajumbe wengi wa chama tawala.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos, amesisitiza kuwa mapendekezo mapya ni muhimu na yamezingatia pia mapendekezo yaliyotolewa na vyama vya upinzani ambavyo vilipinga mkataba huo.