MAREKANI-CUBA-CASTRO

Donald Trump: Fidel Castro alikuwa dikteta katili

Rais wa Cuba Fidel Castro (wakati wa uhai wake) akihutubia umati wa Wacuba Julai 26, 2006 mjini Bayamo, nchini Cuba.
Rais wa Cuba Fidel Castro (wakati wa uhai wake) akihutubia umati wa Wacuba Julai 26, 2006 mjini Bayamo, nchini Cuba. REUTERS/Claudia Daut

Mara baada tu ya serikali ya Cuba kuthibitisha kifo cha Rais wa zamani wa nchi hiyo Fidel Castro, Rais Mteule wa Marekani Donald Trump kuwa mwanamapinduzi huyo wa Cuba alikuwa "dikteta katili".

Matangazo ya kibiashara

Akitangaza kupitia televisheni ya taifa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi Novemba 26, rais wa sasa wa Cuba, ambaye ni kaka wa hayati amesema amiri jeshi mkuu wa mapinduzi ya Cuba amefariki dunia saa nne na dakika 29 usiku.

Bw Trump amesema: "Leo, ulimwengu umeshuhudia kifo cha dikteta katili aliyewakandamiza watu wake kwa karibu miongo sita. Utawala wake ulikuwa wa watu kuuawa kwa kupigwa risasi, wizi, mateso yasiyoweza kufikirika, umaskini na ukiukaji wa haki za kibinadamu."

Donald Trump amesema kuwa anajiunga na raia wengi wa Marekani kutoka Cuba ambao waliomuunga mkono katika kampeni yake ya urais, wakiwemo wale kutoka chama cha maveterani wa Brigade 2506 ambacho kilisahihisha, kwa matumaini kwamba siku moja hivi karibuni tutapata Cuba huru."

"Ingawa Cuba inasalia kuwa kisiwa chini ya utawala wa kiimla, matumaini yangu ni kwamba siku ya leo ni mwanzo wa kuondokea mambo ya kuogofya ambayo yamevumiliwa kwa muda mrefu, na kuelekea siku za usoni ambapo watu wazuri wa Cuba hatimaye wataishi kwa uhuru ambao wanastahili sana."

"Licha ya mikasa na uchungu uliosababishwa na Fidel Castro haviwezi kufutwa, utawala wetu utajaribu kuhakikisha watu wa Cuba wanaanza safari yao kwa ufanisi na uhuru."

 

Rais Barack Obama, ambaye chini ya utawala wake, Marekani ilirejesha uhusiano wa kidiplomasia na Cuba baada ya miongo mingi ya uhasama, amesema historia "Fidel Casro atakumbukwa sana kwa mcango wake katika kufufua uhusiano huo kati ya nchi hizi mbili.

Mkongwe huyo wa mapinduzi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 ambapo mara ya mwisho alionekana hadharani mwezi August.

Fidel Castro aliongoza Cuba chini ya chama kimoja kwa takribani nusu karne kabla ya kukabidhi madaraka kwa kaka yake Raul mnamo mwaka 2008.

Wafuasi wake wanamsifu kwa kuierejesha Cuba mikononi mwa raia licha ya wainzani wake kumshutumu kwa kushughulikia wapinzani kikatili.

Mnamo mwezi April IFidel Castro alitoa hotuba nadra katika siku za mwisho za chama cha kikomunisti.