MAREKANI-SIASA

Trump amteua Jenerali James Mattis kuwa Waziri wa Ulinzi

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Jenerali Mstaafu Jenerali James Mattis kuwa Waziri wake wa Ulinzi.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump akiwa na Jenerali Mstaafu James Mattis aliyemteua kuwa Waziri wa Ulinzi
Rais mteule wa Marekani Donald Trump akiwa na Jenerali Mstaafu James Mattis aliyemteua kuwa Waziri wa Ulinzi
Matangazo ya kibiashara

Trump amemsifu Mattis anayejulikana kwa jina maarufu kama Mad Dog kutokana na umaarufu wake wa kukosoa sera ya rais Barrack Obama kuhusu maswala ya usalama.

Rais huyo mteule amesisitiza kuwa ana imani kubwa kuwa Mattis atafanya kazi nzuri kwa sababu anaamini atakuwa Waziri bora.

Mattis ambaye anafahamika pia kwa kuwa na tabia ya majivuno, amekuwa akikosoa sera ya serikali ya Obama kuhusu ushirikiano wa maswala ya usalama na Iran kwa madai kuwa nchi hiyo inaendelea kuwa hatari kwa usalama wa Marekani.

Baada ya uteuzi huu, bunge la Senate litajadili na kupigia kura uteuzi huu kabla ya Mattis kuanza kazi baada ya Trump kuapishwa mwezi Januari mwaka ujao.

Katika hatua nyingine, Trump ameanza ziara ya kuzunguka katika majimbo mbalimbali yalimsaidia kushinda urais kuwashukuru wapiga kura.

Jimbo la hivi karibuni, kutembelea limekuwa ni lile la Ohio na kuwasifu wakaazi wa jimbo hilo kwa kumpigia kura kwa wingi.