MAREKANI-GUANTANAMO

Wamarekani wajiuliza kuhusu hatma ya jela la Guantanamo

Mwanajeshi wa Marekani mbele ya vyumba vya wafungwa katika sehemu ya 5, katika jela la Guantanamo, Mei 31, 2009.
Mwanajeshi wa Marekani mbele ya vyumba vya wafungwa katika sehemu ya 5, katika jela la Guantanamo, Mei 31, 2009. REUTERS/Brennan Linsley

Katika kisiwa cha Cuba ambaco kimempoteza hivi karibuni kiongozi wake, idadi ya wafungwa katika gereza la Marekani la Guantanamo imeshu, lakini bado kuna wafungwa zaidi ya hamsini ambao wanaendelea kuzuiliwa katika jela hilo. Donald Trump kutoka chama cha Republican, ambaye atamrithi Barack Obama mwezi Januari, anapinga wazo la kufunga jela hilo.

Matangazo ya kibiashara

Katika jela la Guantanamo kunasalia wafungwa hamsini na tisa. Kuhamishwa kwa wafungwa kumi na tisa kulipitishwa. Na Pentagon imeliarifu bunge la Congress kufanyka kwa zoezi la kuhamishwa kwa wafungwa wanane.

Utawala wa Obama umekua ukiharakia kulifunga jela hilo lililo chini ya ulinzi mkali kabla ya kumkabidhi madaraka ya uongozi Donal Trump.

Ahadi hii haitotekelezwa kabla ya Januari 20, lakini Ikulu ya White House inafanya kilio chini ya uwezo wake ili kupunguza idadi hiyo ya wafungwa, lakini kuna baadhi ya wafungwa ambao ni 'hatari' watakaoendelea kuzuiliwa katika jela hilo, hata kama baadhi yao hawakupatikana na hatia.

Wamarekani wengi wamekua na wasiwasi juu ya hatma ya jela la Guantanamo. Donald Trump wakati wa kampeni zake aliahidi, si tu kutofunga jela la Guantanamo, lakini pia kuongeza idadi ya wafungwa katika jela hilo, na kurudisha mateso. Uteuzi wa jenerali Mattis unakuja kushikilia msimamo huu.