SYRIA-UN

Syria ya kwamisha azimio la kusitisha mapigano Syria, kufanya mazungumzo na Marekani

Balozi wa Urusi kwenye umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin.
Balozi wa Urusi kwenye umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin. Bryan Thomas / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP

Urusi inasema itafanya mazungumzo na utawala wa Washington kuhusu uwezekano wa kuondoka kbaisa kwa waasi kwenye mji wa Aleppo, ambako vikosi vya Serikali vimefanikiwa kusonga mbele, lakini upinzani umekataa mpango wa kuondoka.Vikosi vya rais Bashar al-Assad vimechukua karibu robo tatu ya miji muhimu ya waasi mashariki mwa Aleppo, toka Serikali ilipoanza operesheni kuukomboa mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya Urusi, inakuja ikiwa ni saa chache tu zimepita, toka nchi hiyo pamoja na China zitumie kura yao ya turufu kukwamisha azimio la kutoa muda wa siku 7 kusitisha mapigano kwenye mji wa Aleppo.

Venezuela pia ilipiga kura kupinga azimio hili, huku Angola ikijiweka kando na nchi nyingine 11 wanachama zikipiga kura kuunga mkono azimio hili.

Hii ni mara ya sita katika kipindi cha miaka mitano kwa nchi ya Urusi kutumia kura yake ya turufu kukwamisha azimio lolote kuhusu Syria na ikiwa ni mara ya tano kwa nchi ya China kufanya kama Urusi.

Kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria.
Kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria. UN Photo/Eskinder Debebe

Nchi ya Urusi, mshirika wa karibu wa utawala wa rais Assad, ilijaribu kuahirisha kura hiyo hadi siku ya Alhamisi ili nchi ya Urusi na Marekani kukutana mjini Geneva, lakini likagonga mwamba.

Urusi inasema mazungumzo ya Geneva yatahusu uwezekano wa kuwepo makubaliano kwa waasi kuondoka kwenye mji wa Aleppo, mpango ambao hata hivyo tayari upande wa waasi umekataa.