MAREKANI-UGAIDI

Rais Obama azungumzia sera ya ugaidi

Rais Barack amezungumzia na kukemea sera dhidi ya ugaidi na kila kinachopaswa kufanyika katika siku za usoni katika vita dhidi ya ugaidi, ikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya kuachia ngazi katika uongozi wa nchi.

Barack Obama katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, le Novemba 142016.
Barack Obama katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, le Novemba 142016. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Rais Barack Obama amesisitiza kuwa Marekani si nchi ambapo raia anapaswa kutembea na kitambulisho mkononi ili kuonyesha hashukiwi kwa jambo lolote baya au kitendo chochote kiovu . Marekani ni nchi ambayo ilijitolea,i kafanya jitihada kubwa na kujitoa ili kuhakikisha kwamba ubaguzi na sheria kandamizi vinatokomezwa nchini Marekani na Duniani kwa ujumla.

Rais Obama meyasema hayo katika hotuba yake ya mwisho inayohusiana na masuala ya usalama na kueleza kile kilichofanyika katika utawala wake katika nyanja ya usalama.

“Vita dhidi ya ugaidi, havipaswi kupoteza mwelekeo wake na misingi iliyowekwa, “ amesema Rais Obama alipokua akihutubiua askari wake katika kambi ya jeshi la anga ya MacDill ,Tampa, jimboni Florida.

"Marekani taifa linalo amini uhuru wa mtu si jambo linaloweza kuchukuliwa kwa dhana isiyo ya kawaida, na kila mmoja wetu anawajibu wa kuzingatia hilo. Haki ya uhuru wa kusema, kuishi katika jamii iliyo huru na yenye uwazi, na inayoweza kumpinga hata rais ,hivi ni baadhi ya vitu vinavyotu tofautisha na watawala wenye uonevu na magaidi," ameongeza Barack Obama.

Rais Obama amewapongeza wale walichangia kwa hali na mali ili Marekani kuwa mahala salama katika utawala wake.