Watumiaji bilioni 1 wa mtandao wa Yahoo wapoteza anwani zao
Kampuni ya Marekani inayotoa huduma ya Internet ya Yahoo, imesema zaidi ya taarifa za watu Bilioni 1 ziliibwa baada ya watu kuvamia mtandao huo.
Imechapishwa:
Hali hii inaendelea kutishia usalama wa watumiaji wa anwani ya barua pepe ya yahoo katika siku za hivi karibuni baada ya hili kugundulika mwaka 2013.
Kampuni hiyo inasema majina ya watu, namba za simu, namba za siri na anwani za watu ziliibiwa lakini fedha za kampuni hiyo hazikifikiwa.
Watalaam wa Yahoo wamekuwa wakichunguza chanzo cha udukuzi huu, huku uongozi wa kampuni hiyo wakitoa wito kwa watumiaji wa anwani hiyo kubadlisha namba zao za siri.
Yahoo imekuwa ikikosolewa kwa namna inavyoshughulikia swala hili na pia watu wanahoji ni kwanini imewachukua muda mrefu kujitokeza na kuelezea hali hii.