MEXICO-USALAMA

Mexico yaomboleza vifo vya raia wake zaidi ya 30

RONALDO SCHEMIDT / AFP

Mexico inaomboleza vifo vya watu zaidi 30 waliopoteza maisha baada ya kutokea kwa mlipuko katika soko la kuuza fataki na kuwajeruhi wengine zaidi ya 70.

Matangazo ya kibiashara

Madaktari na polisi wamekuwa na kazi nyingi za kuwaokoa na kuwatibu majeruhi wa shambulizi hilo.

Serikali ya Mexico imewambia raia wake wasiende katika soko hilo.

Ripoti zinasema kuwa watoto ndio waliojeruhiwa vibaya na wamesafirishwa kutibiwa nchini Marekani huku watoto waliofariki wakitambuliwa.

Wakati wa shambulizi hilo, kulikuwa na idadi kubwa ya watu katika soko hilo wakifanya manunuzi ya sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.

Ofisi ya mwanasheria Mkuu nchini humo imesema imeanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha mlipuko huo.

Fataki zikifyatuliwa wakati wa sikukuu ya kijadi katika mji wa Tultepec, katika kitongoji cha Mexico cha City, Machi 8 2011.
Fataki zikifyatuliwa wakati wa sikukuu ya kijadi katika mji wa Tultepec, katika kitongoji cha Mexico cha City, Machi 8 2011. Ronaldo Schemidt / AFP