COLOMBIA-ELN-USALAMA

Wapiganaji ishirini wa kundi la waasi la ELN wakamatwa nchini Colombia

Wizara ya Ulizi ya Colombia imetangaza kwamba polisi na jeshi la Colombia waliwakamata Jumapili hii Januari 1 wanachama 20 wa kundi la waasi la ELN, ambalo bado haliweka cini silaha nchini humo.

Wapiganaji wa kundi la waasi la ELN waendelea kukamatwa nchini Colombia.
Wapiganaji wa kundi la waasi la ELN waendelea kukamatwa nchini Colombia. (Photo: Pascal Maitre / Cosmos)
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa operesheni hii katika eneo la Monte Cristo, katika jimbo la Bolivar, polisi "iliwakamata watoto wanane waliokua wakitumiwa na kundi hili," wizara ya Ulinzi imeandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

makubaliano ya amani ya yalisainiwa mwaka uliyopita kati ya serikali ya Colombia na kundi la waasi la FARC ili kumaliza zaidi ya miaka hamsini na mbili ya mapigano.

Bado serikali ya Colombia kuanza mazungumzo ya amani na kundi la waasi la ELN, kundi ambalo halijaweka chini silaha. Kundi hili lenye wapiganaji 1,500 lilianza vita vya maguguni kama FARC mwaka 1964 na bado halijakubali kusitisha mapigano na serikali ya Colombia.

Serikali ya Bogota inaomba kuachiliwa kwa Mbunge wa zamani Odin Sanchez, anayeshikiliwa tangu Aprili na kundi la ELN kabla ya kuanza mazungumzo ya amani ambapo majadiliano ya awali yanatazamiwa kuanza tarehe 10 Januari 2017.