CHILE-MAJANGA YA ASILI

Moto mkubwa wateketeza msitu karibu na mji wa Valparaiso

Moto mkubwa ulianza Jumatatu katika vijiji mbalimbali vya mkoa wa Valparaiso, na kuteketeza nyumba nyingi, huku watu 19 wakijeruhiwa, kwa mujibu wa serikali ya Chile.

Moto mkubwa waukumba mkoa wa Valparaiso tangu Januari 2, 2016 na tayari umeteketeza hekta 50 za msitu.
Moto mkubwa waukumba mkoa wa Valparaiso tangu Januari 2, 2016 na tayari umeteketeza hekta 50 za msitu. Francisco Venegas / AFP
Matangazo ya kibiashara

Moto huo ullizuka kusini mwa mkoa wa Valparaiso, katika wilaya ya Laguna Verde, kisha ulienea katika eneo la Playa Ancha, na kuharibu "nyumba 100 kati ya 500 'zilizojengwa katika eneo hilo, amesema Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mahmud Aleuy katika mkutano na waandishi wa habari mjini Santiago.

Watu kumi na tisa walijeruhiwa, wengi wao wakiwa na matatizo ya kupumua, lakini "kwa bahati nzuri hakuna mtu aliyefariki," bw Aleuy ameongeza.

Hekta hamsini tayari zimeteketezwa kwa moto, kulingana na taarifa za awali kutoka Idara ya Taifa ya Dharura (Onemi).

Joto liliyo kwenye kiwango cha juu na upepo mkali vimesababisha moto huo kuenea katika maeneo mbalimbali ya mji.

Watu 200 wamehamishwa na shirika la umeme lililazimika kuwakatia umeme, kwa tahadhari, watu karibu 48,000 wanaoutumia.