MAREKANI-USALAMA-UGAIDI

Marekani yamsaka mwana wa Osama Bin Laden

Osama Bin Laden, baba wa Hamza Bin Laden anayetafutwa na Marekani.
Osama Bin Laden, baba wa Hamza Bin Laden anayetafutwa na Marekani. REUTERS/Pentagon/Handout

Marekani imetangaza kwamba imemuorodhesha mwana wa mwisho wa Osama Bin Laden Hamza katika orodha ya magaidi wanaosakwa na taifa hilo, baada ya kukiri kuwa atalipiza kisasi mauaji ya babake.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Idara ya maswala ya kigeni, Hamza Bin Laden ameanza kushiriki katika harakati za kundi la al Qaeda, kundi la Waislamu wenye msimamo mkali lililofadhiliwa na babake, Osama bin Laden.

Hamza Bin Laden amesema kuwa atalipiza kisasi mauaji ya babake yaliotekelezwa na kikosi cha askari maalum wa Marekani nchini Afghanistan.

Marekani imesema kuwa mtoto huyo wa mwisho wa Osama Bin Laden atapigwa marufuku kwa kufanya biashara na raia wa Marekani, na mali yake ikitazuiliwa.

Mkuu wa kitengo cha usalama cha kundi la al-Qaeda Ibrahim al-Banna pia amewekwa katika orodha hiyo ya magaidi wanaosakwa na Marekani.

Tayari Marekani imetoa kitita cha dola milioni 5 kwa mtu yeyote atakayemkamata Ibrahim al-Banna.