MAREKANI

Wabunge wa Republicans na Democrats wajiandaa kupambana kuhusu sera ya afya ya Obamacare

Rais wa Marekani Barack Obama, ametoa wito kwa wabunge wa chama cha Democrats "kupambana" kuhakikisha saini yake kuhusu mabadiliko yake ya mfumo wa afya nchini inabaki, wakati huu rais mteule Donald Trump na wabunge wa chama chake wakitaka kuifanyia marekebisho sheria hiyo.

Kinara wa wachache bungeni kutoka Democrats, Chuck Schumer, akihutubia baada ya mkutano wao wa kwanza kuhusu mpango wa afya wa Obama, Januari 4, 2017
Kinara wa wachache bungeni kutoka Democrats, Chuck Schumer, akihutubia baada ya mkutano wao wa kwanza kuhusu mpango wa afya wa Obama, Januari 4, 2017 REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

"Obamacare", matunda ya miaka minne ya utawala wake kuhakikisha huduma za matibabu zinapanuliwa kwa kila mtu na mamilioni ya raia wa Marekani, mpango huu sasa uko kwenye mashaka makubwa ya kuendelea kuwepo kutokana na mikakati ambayo rais mteule Trump anayo kuhakikisha anaubadilisha wakati atakapoingia ofisini Januari 20, huku chama chake kikiongoza mabunge yote mawili, Seneti na Congress.

Hata hivyo mjadala mkali tayari umeanzia katika ngazo za juu za uongozi wa vyama vya Republican na Democrats, huku rais Obama na makamu wa rais mteule Mike Pence wote wakifanya ziara katika ofisi za Capitol Hill kuwashawishi wabunge wao kujiandaa kwa lolote.

Rais wa Marekani Barack Obama wakati akiingia katika majengo ya bunge "Capitol Hill" Januari 4, 2017
Rais wa Marekani Barack Obama wakati akiingia katika majengo ya bunge "Capitol Hill" Januari 4, 2017 REUTERS/Kevin Lamarque

"Nawasihi ninyi mliopata nafasi hii ambayo mtajumuika katika kuizungumza na kupambana kuhakikisha mfumo huu unalindwa kwaajili ya wamarekani," alisema Seneta wa democrats Ed Markey ambaye alihudhuria kikao kilichodumu kwa dakika zaidi ya 100.

Baada ya kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa mwaka jana, wabunge wa Democrats wanayo nafasi finyu sana ya kulinda mpango huu wa afya hasa ikiwa hakutakuwa na wabunge wa Republican ambao watawaunga mkono.

Republicans wanadai kuwa mfumo wa afya wa Obamacare, umesababisha kupanda wa huduma za bima pamoja na kuwa na matatizo mengi ya kiufundi.

Hata hivyo licha ya juhudi zao, bado mpango wa Obamacare umesalia kuwa maarufu kwa wamerekani wengi ambao punde baada ya kutiwa saini kuwa sheria, uliwezesha raia wengi zaidi kuweza kupatiwa matibabu huku watoto wakitibiwa hadi kufikia umri wa miaka 26.