MAREKANI-URUSI-UCHAGUZI

Serikali ya Marekani yawatambua mawakala wa Urusi walioingilia uchaguzi wa Marekani

Donald trump, rais mteule wa Marekani.
Donald trump, rais mteule wa Marekani. REUTERS/Lucas Jackson

Ripoti zinasema kuwa Marekani imeshawafahamu mawakala wa Kirusi wanaotuhumiwa kuingilia Uchaguzi wa Marekani, uliompa ushindi Donald Trump mwezi Novemba mwaka uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Inaaminika kuwa mawakala hao ambao hawajatambuliwa kwa majina, waliiba taarifa muhimu kutoka barua pepe ya chama cha Democratic na kuipa mtandao wa Uchuguzi wa Wikileaks ili kumsaidia Trump kushinda Uchaguzi.

Makamu wa rais anayemaliza muda wake Joe Biden amemsuta Trump kama rais ambaye hajakomaa na hachukulii suala hili kwa uzito.

Urusi imekanusha madai ya kuingilia Uchagizi wa Marekani pamoja na Trump ambaye anatarajiwa kuapishwa baadaye mwezi huu, amesema madai hayo sio kweli.