UN-GUTERRES-HOTUBA-AMANI

Katibu Mkuu mpya wa UN apendekeza mabadiliko katika utaratibu wa kusaka amani

Antonio Guterres mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumanne, Januari 10, 2017.
Antonio Guterres mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumanne, Januari 10, 2017. REUTERS/Stephanie Keith

Baada ya kuchukua hatamu ya uongozi Januari 1, 2017, Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa Jumanne hii, Januari 10 hotuba yake ya kwanza mbelea ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Matangazo ya kibiashara

Wanadiplomasia wamefurika kwa wiki kwa kuja kusikiliza hotuba ya kwanza ya Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa. Antonio Guterres alisikilizwa kwa umakini kuhusu jukumu ya Umoja wa Mataifa katika kuzuia migogoro.

 Hotuba hii ya kwanza itatoa maelekezo ya wazi kwa ajili ya Taasisi hiyo ya kimataifa. Lakini Guterres amerejelea hoja mbalimbali alizotamka wakati alipotawazwa. "Kuzuia migogoro inapaswa kuwa kipaumbele cha Umoja wa Mataifa," alisema. Umoja wa Mataifa unatumia muda zaidi kwa kusimamia migogoro badala ya kuzuia, amesema Antonio Guterres ambaye ametetea mabadiliko katika utaratibu wa kusaka amani.

Katibu Mkuu mpya amependekeza kuweka mbele malengo ya maendeleo endelevu, mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, ambayo ni mambo yanayosababisha migogoro. Kwa upande wa Umoja wa Mataifa, pia ameahidi kubadili utaratibu. Kufuatia hali hiyo, tayari ameunda kamati tendajiitakayokua ikimpa ripoti kila wiki. Pia ameahidi kufanya juhudi ya kuhamasisha upatanishi wa kikanda na kimataifa, ambapo amepania kuwekeza mwenyewe ili mwaka 2017 uwe "mwaka wa amani."