MAREKANI

Joe Biden atunukiwa medali ya heshima na rais Obama

Rais wa Marekani Barrack Obama, amemtunuku Makamu wake Joe Biden nishani ya hadhi ya juu anayoweza kupewa raia wa taifa hilo kutambua utendaji wake.

Joe Biden akitunukiwa medali ya heshima na rais Barrack Obama.
Joe Biden akitunukiwa medali ya heshima na rais Barrack Obama. www.hellomagazine.com
Matangazo ya kibiashara

Obama amesema, Biden anastahili kupata Medali hiyo ya Uhuru kwa sababu ya kazi nzuri aliyowafanyia raia wa Marekani kwa muda mrefu, lakini pia kutekeleza ipasavyo majukumu yake kama Makamu wake kwa muda wa miaka nane iliyopita.

Biden ambaye alishangazwa na hatua hiyo, alitokwa na machozi wakati rais Obama alimpomtunuku medali hiyo na kusema hakutarajia kupewa heshima hiyo.

Tuzo hii imekuja wakati huu viongozi hawa wanapoajindaa kuondoka madarakani tarehe 20 mwezi Januari, baada ya kuapishwa kwa rais mteule Donald Trump.

Obama na Biden wamekuwa wakisifiwa na wachambuzi wa siasa nchini humo na kwingineko duniani kama, viongozi waliofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

Biden ameahidi kuendelea kujihusisha na siasa ndani ya chama cha Democratic katika miaka ijayo.