MAREKANI-CUBA-USHIRIKIANO

Marekani: raia wa Cuba kulipa visa

Rais wa Cuba watakua wajkilipa visa kwa kuingia nchini Marekani.
Rais wa Cuba watakua wajkilipa visa kwa kuingia nchini Marekani. © RFI/Véronique Gaymard

Marekani imefuta sera ya muda mrefu iliokuwa inawapa raia wa Cuba fursa maalumu ya kuingia na kuishi nchini Marekani bila ya visa.

Matangazo ya kibiashara

Rais Obama amebaini kuwa hatua ya kuondolewa kwa sera hiyo, ni hatua muhimu katika kurudisha uhusiano na Cuba.

Hata hivyo serikali ya Cuba imekuwa ikilalamika kwamba, sera hiyo, ijulikanayo kama "wet foot, dry foot," imewafanya maelfu ya raia wa Cuba kukimbia nchi yao kila mwaka na kuelekea nchini Marekani

Mwaka 2015 nchi hizi mbili zilirudisha uhusiano wa kidiplomasia baada ya miaka karibu 100 ya uhasama.

Hata hivyo uhusiano huo umeanza kukosolewa na rais mteule wa Marekani Donald Trumpe mwezi huu anakabidhiwa madaraka ya uongozi wa nchi.

Ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa urais nchini Marekani ulipokelewa na wasiwasi na Wacuba wengi. Kwa uhakika, wanahofia kuona juhudi za kufufua uhusiano kati ya nchi yao na Marekani zinaweza kuambulia patupu.

Uchaguzi wa Donald Trump umesababisha raia wengi wa Cuba kukata tamaa. Donald Trump alipozuru Florida tarehe 21 Oktoba, wakati alikuwa bado mgombea, alikutana na wapinzani wa utawala wa kikomunisti wa Cuba na alisema anawaunga mkono kwa harakati zao.