MAREKANI-TRUMP-SERA ZA NJE

Donald Trump afafanua sera zake za kigeni

Trump amemkosoa kansela wa Ujerumani Angela Merkelakisem akuwa alifanya kosa kubwa kwa wakimbizi wengi kutoka Syria na mataifa mengine kuingia nchini Ujerumani.
Trump amemkosoa kansela wa Ujerumani Angela Merkelakisem akuwa alifanya kosa kubwa kwa wakimbizi wengi kutoka Syria na mataifa mengine kuingia nchini Ujerumani. REUTERS/Lucas Jackson

Rais mteule wa Marekani Donald Trump, ameelezea kuhusu masuala muhimu ambayo yanatakiwa kugshughulikiwa haraka katika sera zake za kigeni. Bw Trump amesema hayo katika mahojiano na gazeti la Times la Uingereza na gazeti la Bild la Ujerumani.

Matangazo ya kibiashara

Katika uongozi wake Bw Trump amezungumzia akisisitiza juu ya suala la biashara yenye tija zaidi kuliko biashara huru.

Trump amesema anataka mipango ya biashara yenye usawa kwa Marekani kutoa mipango yake ya biashara na nchi nyingine duniani hususani China.

Rais mteule wa Marekani amesema kuwa kampuni kubwa za kibiashara nchini Marekani zilizowekeza nje ya Marekani zitakabiliana na ushuru mkubwa wa bidhaa wanazotaka kuuza nchini Marekani.

Trump amemkosoa kansela wa Ujerumani Angela Merkelakisem akuwa alifanya kosa kubwa kwa wakimbizi wengi kutoka Syria na mataifa mengine kuingia nchini Ujerumani.

Trump amesema kwamba angependa Urusi na Marekani wakubaliane kupunguza kwa kiasi kikubwa silaha za nyuklia kwa kubadilishana na kusitisha vikwazo vinavyoikabili Urusi.

Bw Trump pia amesema mahusiano mazuri yangetakiwa kuundwa nchini Syria na kusimamiwa na washirika wa Marekani.

Trump amepongeza Uingereza akisema wamefanya vizuri kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya.