MAREKANI-OBAMA-MSAMAHA

Obama awasamehe wanajeshi kwa mara ya mwisho

Barack Obama akitoa hotuba yake ya mwisho kama Rais wa Marekani Jumanne, Januari 10, 2017.
Barack Obama akitoa hotuba yake ya mwisho kama Rais wa Marekani Jumanne, Januari 10, 2017. REUTERS/Carlos Barria

Rais Obama amechukua uamuzi wa kubatilisha kifungo alichohukumiwa Chelsea Manning, aliyekuwa mwanajeshi wa Marekani ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la kufichua nyaraka za siri.

Matangazo ya kibiashara

Mwanajeshi huyo aliyekuwa mwanamageuzi aliyefanya kazi nchini Iraq alikuwa akijulikana pia kama Bradley Manning.

Picha ya  Chelsea Manning akijulikana kama Bradley Manning ya mwaka 2010 akijifananisha na mwanamke.
Picha ya Chelsea Manning akijulikana kama Bradley Manning ya mwaka 2010 akijifananisha na mwanamke. REUTERS/U.S. Army/Handout

Alikutwa na hatia ya kufichua nyaraka za siri mwaka 2013 kwa kuweka karibia robotatu ya mamilioni ya nyaraka za siri za kijeshi na kidiplomasia katika tovuti ya WikiLeaks.

Taarifa kutoka ikulu zinasema Manning ataachiwa huru ifikapo mwezi wa tano.

Rais Obama pia ametoa msamaha kwa aliye kuwa afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Maekani Jenerali James Cartwright, aliyekubali kosa la kutoa taarifa za uongo katika uchunguzi uliokuwa ukifanywa na FBI katika udukuzi wa compyuta kuhusu mipango ya kinyuklia ya Iran.

Uamuzi huo unakuja ikiwa zimesalia siku chache tu ili rais Barack Obama amkabidhi madaraka ya uongozi wa nchi mrithi wake Donald Trump aliyeshinda uchaguzi wa urais wa mwaka jana.