MAREKANI-WIKILEAKS-MSAMAHA

WikiLeaks: Julian Assange yuko tayari kurejea Marekani

Mwanzilishi wa WikiLeaks, Julian Assange, yuko tayari kusafiri kwenda Marekani, ambapo anakabiliwa na tuhuma nzito, kama haki zake zitaheshimishwa, tovuti yake imetangaza Jumatano hii Januari 18.

Julian Assange aomba haki zake ziheshimishwe ili aweze kurudi Marekani.
Julian Assange aomba haki zake ziheshimishwe ili aweze kurudi Marekani. REUTERS/John Stillwell/pool
Matangazo ya kibiashara

"Bw Assange yuko tayari kusafiri kwenda Marekani ikiwa haki zake zitazingatiwa, " WikiLeaks imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, na kunukuliwa na shirika la habari la AFP.

Tangazo hili linakuja baada ya uamuzi wa Barack Obama kupunguza hukumu ya Chelsea Manning,aliyehukumiwa katika miaka ya 2013 kifungo cha miaka 35 gerezani kwa kosa la kufichua nyaraka za siri 700,000 kwa WikiLeaks.

Chelsea Manning, akijulikana kwa jina la Bradly Manning iataachiwa huru Mei 17.

Wiki iliyopita, WikiLeaks ilitangaza kwamba Assange angelikubali kusafirishwa nchini Marekan kama rais wa Marekani atamsamehe Chelsea Manning.

Lakini maafisa kutoka Ikulu ya White House wamesema kuwa hakuna uhusiano kati ya ujumbe huu na uamuzi wa Barack Obama.

Julian Assange alikimbilia katika Ubalozi wa Ecuador mjini London tangu mwezi Juni 2012 kwa kuepukakusafirishwa nchini Sweden ambapo anakabiliwa na mashtaka ya ubakaji, mashitaka ambayo ameendelea kukanusha.