MAREKANI-TRUMP-UHAMIAJI

Makampuni kadhaa ya Marekani yalaani agizo la Donald Trump dhidi ya wahamiaji

Agizo la Donald Trump ambalo linapiga marufuku raia kutoka mataifa mengi ya Mashariki ya Kati kuingia nchini Marekani limezua hali ya sintofahamu katika makampuni ya Silicon Valley. Makampuni ya teknolojia mpya yanaajiri idadi kubwa ya vijana wenye vipaji kutoka katika ukanda huo.

Mamia ya waandamanaji wameandamana kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa JFK wakipinga sera ya uhamiaji ya Donald Trump inayopiga marufuku wahamiaji kuingi anchini Marekani, Januari 28, 2017.
Mamia ya waandamanaji wameandamana kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa JFK wakipinga sera ya uhamiaji ya Donald Trump inayopiga marufuku wahamiaji kuingi anchini Marekani, Januari 28, 2017. REUTERS/Stephen Yang
Matangazo ya kibiashara

Waajiri wa Silicon Valley wamechukua uamuzi wa kupinga dhidi agizo la rais Trump ambalo linapiga marufuku wahamiaji nchini Marekani. Hata kampuni ya Twitter, moja ya mitandao ya kijamii anayotumia Rais wa Marekaniimesem ainaunga mkono wahamiaji.

Wkurugenzi Wakuu wa Apple, Facebook, Netflix, Google na Microsoft wanakubaliana katika kulaani kikwazo hiki kwa kuajiri wahandisi wengi katika sekta hii kutoka nchi zilizolengwa na agizo la rais Donald Trump.

Apple, kampuni ilioanzishwa na Steve Jobs, mtoto wa mhamiaji kutoka Syria, "haitokuwepo bila wahamiaji," amesema Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Tim Cook. Mmiliki wa kampuni ya Netflix , kwa upande wake ametoa wito wa kulinda maadili ya Marekani ya uhuru na nafasi. "Hatua za Trump zinaathiri wafanyakazi wa kampuni ya Netflix duniani kote ... Ni wakati wa kujiunga pamoja na kulinda maadili ya Marekani ya uhuru na nafasi," Reed Hastings ameandika kwenye akaunti yake ya Facebook.

Microsoft, kwa upande wake, inasema kwamba hali hii itaizuia kujaza nafasi zote zilizo wazi katika timu za utafiti na maendeleo. Takriban wafanyakazi 187 wa kampuni ya Google wanaathirika na vikwazo hivi vipya, amesema kwenye barua pepe ya kamupuni hiyo Sundar Pichai, Mkurugenzi mkuu wa Google.

Eloni Musk, mwanzilishi wa kampuni ya Tesla na SpaceX ambaye hivi karibuni alikutana na Donald Trump, amebaini kwenye Twitter kwamba "marufuku ya jumla kwa wananchi kutoka nchi kadhaa za Kiislamu kuingia nchini Marekani si njia bora ya kukabiliana na changamoto " zinazonatokea.

Kwa upande wa mmiliki wa Microsoft, mwenye asili ya India, amesema, kama wmhamiaji na kama Mkurugenzi Mkuu, athari chanya ya uhamiaji.

Itafahamika kwamba agizo la kupiga marufuku raia kutoka nchi saba za Kiislamu kuingia nchini Marekanililisababisha mikusanyiko na maandamano ya hasira nchini kote, siku moja baada ya krais Donald Trump kutia saini kwenye agizo hilo. Zaidi ya watu 2000 walivamia na kuandamana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John Fitzgerald Kennedy, huku wakidai kuachiwa huru kwa watu waliozuiliwa kwenye idara ya Forodha. Wakati huo huo, jaji wa mjini New York aliomba kuachiliwa kwa wasafiri wote waliokua na visa halali.