MAREKANI-TRUMP-UHAMIAJI

Trump atetea sera yake ya usafiri

Maelfu ya Waandamanaji wapinga dhidi ya amri ya Donald Trump inayopiga marifuku Waislamu kutoka nchi saba za Mashariki ya Kati kuingia Marekani, Januari 29, 2017 Washington DC.
Maelfu ya Waandamanaji wapinga dhidi ya amri ya Donald Trump inayopiga marifuku Waislamu kutoka nchi saba za Mashariki ya Kati kuingia Marekani, Januari 29, 2017 Washington DC. REUTERS/Aaron P. Bernstein

Rais wa Marekani Donald Trump ametetea agizo alilolitoa ambalo inapiga marufuku watu wanaotoka katika nchi saba ambazo ni za kiislamu kuingia nchini Marekani. Uttetezi wake huo unakuja baada ya watu kuukosoa uamuzi huo huku wengine wakiandamana.

Matangazo ya kibiashara

Rais Donald Trump amevilaumu vikali vyombo vya habari akisema kwamba vimepotosha taarifa kwamba marufuku hiyo inawalenga tu Waislamu.

Hata hivyo Reince Priebus, ambae ni kiongozi wa wafanyakazi wa serikali amesema agizo hilo la Trump halitawahusu watu wenye kuhodhi kadi za green, ambao wana haki ya kisheria kuishi nchini Marekani.

Wadadisi wanasema kwamba tayari inaoonekana kuwa utawala wa Trump umeanza kulegeza msimamo wa amri ya kiutendaji iliyopitishwa siku ya Ijumaa. Na hali hiyo huenda ikapelekea utawala huo kuendelea kudhoofika.

Washauri wakuu wa masuala ya sheria kutoka majimbo kumi na sita nchini Marekani wameshutumu marufuku hiyo ya kusafiri na kusema haiko kisheria, imekiuka maadili ya kimarekani na imekiuka katiba ya nchi.

Wakati huo huo, maelfu ya waandamanaji wanaopinga agizo hilo la Trump wameandamana kwa mara nyengine katika viwanja vya ndege na maeneo mengine nchini Marekani.

Waandamanaji wamepita katika miji ya Boston, New York na karibu na ikulu mjini Washington.