Donald Trump amtimua mwanasheria mkuu
Imechapishwa:
Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa chache baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini Marekani kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika mataifa saba ya kiislamu.
Sally Yates ambaye Taarifa ya Ikulu ya White House imemshtumu kwa usaliti aliteuliwa na Obama. Ahata hivyo alisema kuwa haamini kwamba marufuku hiyo ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni sahihi.
Agizo la rais la kupiga marfuku raia kutoka mataifa saba ya Kiislamu kuingia nchini Marekan lililtiwa saini Ijumaa iliopita, na tayari limesababisha maandamano nchini Marekani.
Wadhfa Sally Yates umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo mjini Virginia Dana Boente.