MAREKANI-TRUMP-SERA ZA NJE

Obama apongeza uhamasishaji dhidi ya agizo linalopiga marufuku wahamiaji

Siku kumi baada ya kukamilika rasmi kwa muhula wake wa mwisho, Barack Obama (hapa ilikua Desemba 6, 2016) aonyesha msimamo wake.
Siku kumi baada ya kukamilika rasmi kwa muhula wake wa mwisho, Barack Obama (hapa ilikua Desemba 6, 2016) aonyesha msimamo wake. MANDEL NGAN / AFP

Siku kumi baada ya kutawazwa kwai mrithi wake Donald Trump, Obama ameonyesha msimamo wake juu ya masuala nyeti, yanayoshuhudiwa nchini Marekani wakati huu. Amri ya kuzuia raia kutoka nchi 7 kusafiri Marekani kwa kipindi cha siku 90 imezua hali ya sintofahamu na mkanganyiko nchini Marekani na kupelekea wananchi wengi kuanza kujuta.

Matangazo ya kibiashara

Barack Obama amethibitisha kuwa hatoingiliakati katika mjadala wa kisiasa isipokuwa iwapo Donald Trump atakaua amevuka baadhi ya maeneo hatari. Bw Obama alikuwa alisema wakati wa mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari Januari 18 vigezo ambavyo vinaweza kupelekea kuingilia kati: ubaguzi wa aina yoyote, vikwazo vya upigaji kura, majaribio ya kunyamazisha wapinzani au vyombo vya habari, au wazo la kufukuza watoto ambao walikulia katika ardhi ya Marekani.

Barack Obama ameamua kuweka wazi msimamo wake kupitia afisa wake anayehusika na mawasiliano na yombo vya habari Kevin Lewis. Katika taarifa iliotumwa na Kevin Lewis, Barack Obama amepongeza Wamarekani kwa kuandamana kwa minajili ya kulinda demokrasia na amekaribisha kiwango cha ushiriki katika uhamasishaji nchini kote. "Ukweli ni kwamba wananchi wanatumia haki yao ya kikatiba ya kukusanyika, ya kuhamasisha na ya kusikilizwa na wawakilishi wao ni sawa na kuingilia kati wakati maadili ya Marekani yanakua hatarini," amesema Bw Obama.

Bila hata kutaja jina la Donald Trump, taarifa hiyo imebainia kwamba rais Obama hakukbaliani na tabia ya kuwabagua watu kwa sababu ya imani au dini."

Tangu kusainiwa kwa amri kufunga milango ya Marekani kwa wakimbizi na raia wa nchi saba za Kiislamu kwa kipindi cha miezi mitatu, Rais Donald Trump ameendelea kukosolewa kutoka pande zote duniani, nje ya nchi sawa na nchini Marekani. Kwa mujibu wa Barack Obama, hatua hii inakwenda kinyume na maadili ya kimsingi ya Marekani. Maadili ambayo, kwa sasa yamewekwa hatarini, ameongeza barack Obama.