BRAZIL-USALAMA

Nchini Brazil, baadhi ya polisi warejea kazini

Askari polisi zaidi ya 1,200 kutoka jimbo la Espirito Santo nchini Brazil waliamua kurejea kazini siku ya Jumapili na kusitisha mara moja ushiriki wao katika mgomo ulioanza tangu wiki iliyopita. Mgomo ambao ulisababisha kuongezeka kwa vurugu na uhalifu katika eneo la kaskazini mwa mji wa Rio de Janeiro.

Kwa mujibu wa chama cha polisi, visa 144 vya mauaji vilitekelezwa tangu kuzuka kwa mgomo huo Februari 4, katika jimbo la Espirito Santo,Februari 9, 2017.
Kwa mujibu wa chama cha polisi, visa 144 vya mauaji vilitekelezwa tangu kuzuka kwa mgomo huo Februari 4, katika jimbo la Espirito Santo,Februari 9, 2017. REUTERS/Paulo Whitaker
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya askari 3,100 na askari wa kikosi cha ulinzi wa rais walitumwa katika jimbo hilo kurejesha hali ya utulivu. Jimbo la Espirito Santo lilishuhudiwa maukio ya uporaji kwa sababu mgomo wa polisi, ambao walikua wakidai nyongezo ya mshahara.

Polisi 10,000 wanakataa bado kurejea kazini.

Kiwango cha uhalifu kilieongezeka mara sita katika wiki chache zilizopita wakati ambapo maduka yalifungwa, na shughuli kuzorota katika mashule na hospitali.

Vurugu nyingi zilishuhudiwa katika maeneo a watu maskini ya Vitoria, mji mkuu jimbo la espirito Santo ambapo wanaishi wakazi milioni mbili wanaoishi kwa rasilimali zinazohusiana na madini, mafuta na shughuli za bandarini.

Kwa mujibu wa chama cha polisi, visa144 vya mauaji vilitekelezwa tangu kuzuka kwa mgomo huo Februari 4, ambavyo hasavilihusiana na biashara ya madawa ya kulevya, ingawa wapita nia kadhaa pia waliuawa.