PERU-MAREKANI

Pedro Pablo: Nivema Trump kumsalimisha rais Toledo

Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski amemuombarais wa Marekani Donald Trump kumsalimisha rais wa zamani wa Peru Alejandro Toledo ambaye anatafutwa na mahakama ya Peru kujibu mashitaka ya rushwa yanayomkabili.

Hati ya Kimataifa ya kukamatwa kwa rais wa zamani wa Peru Alejandro Toledo na zawadi ya Euro 29,000  imeahidiwa kwa yeyote atakayetoa habari zitakazosaidia kukamatwa kwake.
Hati ya Kimataifa ya kukamatwa kwa rais wa zamani wa Peru Alejandro Toledo na zawadi ya Euro 29,000 imeahidiwa kwa yeyote atakayetoa habari zitakazosaidia kukamatwa kwake. Peruvian Police/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Bw Toledo, ambaye inaaminika kwa sasa yupo mjini San Francisco, anatuhumiwa kupokea rushwa ya jumla ya Dola milioni 20 (sawa na Euro milioni 16).
Hata hivyo rais wa zamani wa Peru Alejandro Toledo amekanusha tuhuma hizo.

Rais Kuczynski akizungumza na rais wa Marekani Donald Trump alimuomba kumsalimisha kiongozi huyo wa zamani wa Peru ili ajibu mashitaka yanayomkabili.

Marekani imesema haiwezi kumkamata kiongozi huyo wa zamani hadi maelezo zaidi kuhusu kesi inayomkabili yawasilishwe kwake na maafisa wa Peru.

Kufikia sasa, juhudi za kumkamata Bw Toledo zimekwama kutokana na changamoto za kisheria.

Hayo yakijiri Israel ilitangaza Jumapili hii kwamba haitompokea kwenye ardhi yake rais wa zamani wa Peru Alejandro Toledo, anayetafutwa na mahakama ya nchi yake kwa kosa la rushwa.

"Bw Toledo ataruhusiwa (kuingia) katika kardi ya Israel pale tu kesi yake itakua imeshughulikia na vyombo vya sheria vya nchi yake," Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Israel, Emmanuel Nahshon.

Serikali ya Peru ilisema Ijumaa Februari 10 kwamba ina taarifa kwamba rais wa zamani wa Peru, ambaye mkewe ni raia wa Israel, amekua akijaribu kukimbilia nchini Israeli. Awali alikua kitaka kukimbilia katika mji wa Paris nchini Ufaransa.

Wizara ya mambo ya nje ya Israel imesema Bw Toledo hataruhusiwa kuingia nchini humo hadi "masuala yanayomhusu Peru yahitimishwe."

Zawadi ya zaidi ya Dola 30,000 (sawa na Euro 29,000) imeahidiwa kwa yeyote atakayetoa habari zitakazosaidia kukamatwa kwa Bw Toledo.