VENEZUELA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Nicolas Maduro: Marekani yapaswa kuomba msamaha

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ameitaka marekani kuomba msamaha na kuondoa vikwazo dhidi ya makamu wake, Tareck el-Aissami anaeshutumiwa na Marekani kwa kuhusika na ulanguzi wa mihadarati.

Nicolas Maduro amuunga mkono Makamu wake, TareCk el-Aissami, anaekabiliwa na vikwazo vya Marekani. Caracas, Februari 14, 2017..
Nicolas Maduro amuunga mkono Makamu wake, TareCk el-Aissami, anaekabiliwa na vikwazo vya Marekani. Caracas, Februari 14, 2017.. Miraflores Palace/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tareck el-Aissami amewekewa vikwazo vya kuzuiwa mali yake nchini Marekani na pia amepigwa marufuku kuingia au kufanya ziara yoyote nchini humo.

Tareck el-Aissami amekuwa akitangazwa kama mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika chama tawala.

Wizara ya fedha Marekani ilisema Tareck el-Aissami ni mlanguzi mkuu wa dawa za kulevya na amekuwa akifanya kazi na walanguzi Mexico na Colombia kusafirisha mihadarati hadi Marekani.

Bw Maduro amesema hatua ya Marekani ni kama uchokozi usiokua na msingi na amesem aakisisitiza kuwa anamuunga mkono kwa dhati Bw el-Aissami .

Itafahamika kwamba Marekani na Venezuela haziajakuwa na uhusiano wa kibalozi tangu 2010.