Mike Pence atumia anwani yake binafsi
Imechapishwa:
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence amejikuta katika kashafa ya kutumia anwani yake binafsi kufanya kazi za kiofisi alipokuwa Gavana wa jimbo la Indiana.
Imebainika kuwa alitumia anwani kujadili maswala muhimu na ya siri kuhusu kuhusu usalama kinyume na utaratibu wa kazi.
Haya yote yamebainika baada ya anwani yake kudukuliwa mwaka uliopita.
Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anamwamini Mwanasheria Mkuu Jeff Sessions kama mtu mwadilifu na mkweli licha ya shinikizo za kumtaka kujiuzulu.
Shinikizo za kujiuzulu kwa Sessions zinatolewa na wabunge hasa wa chama cha Democratic wanaosema alishuhudia uongo baada ya kubainika kuwa alikutana na Balozi wa Urusi nchini humo wakati akiwa Seneta kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka uliopita.