MAREKANI-TRUMP-WAHAMIAJI

Trump kusaini Jumatatu agizo lake jipya kuhusu wahamiaji

Jumatatu wiki hii Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kusaini agizo lake jipya kuhusu wahamiaji, agizo ambalo lilizuiliwa na mahakama baada ya kuzua hali ya utata mkubwa na kusababisha machafuko katika viwanja vya ndege, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani.

Donald Trump kusaini agizo jipya kuhusu wahamiaji kwenye Wizara ya Usalama wa Ndani.
Donald Trump kusaini agizo jipya kuhusu wahamiaji kwenye Wizara ya Usalama wa Ndani. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Rais atasaini agizo jipya kuhusu wahamiaji kwenye Wizara ya Usalama wa Ndani, kwa mujibu wa gazeti la Politico, likinukuu maafisa wa nagazi ya juu serikalini.

Haikuwezekana kujua kile ambacho Donald Trump alipangilia kuingiza katika rasimu hii mpya, kwa mujibu wa gazeti hili lenye utaalamu katika maswala ya kisiasa.

Manunguniko dunini kote

Agizo la Januari 27, linalopiga marufuku raia kutoka nchi saba za Kiislamu kuingia nchini Marekani kwa siku 90, na lile la wakimbizi wote kwa siku 120, na lile la wakimbizi wa Syria kutoingi kabisa nchini Marekani.

Baada ya kuzua hasira duniani kote na wimbi la maandamano nchini Marekani, agizo hilo lilisababishwa machafuko katika viwanja vya ndege.

Rais wa Marekani alikabiliwa hatua mbili muhimu za mahakama kuhusuagizo lake la Januari 27. Februari 3, Jaji wa Seattle, kaskazini Magharibi mwa Marekani alizuia utekelezaji wa agizo hilo. Mnamo Februari 9, Mahakama ya Rufaa ya San Francisco, magharibi mwa nchi hiyo iliomba hatua ya Jaji wa Seattle izingatiwe.