MAREKANI-TRUMP-OBAMA

White House yaomba Bunge la Congress kuchunguza kile alichokifanya Obama

Marais Barack Obama na Donald Trump, Januari 20, 2017 wakati wa kukabidhiana madaraka mjini Washington.
Marais Barack Obama na Donald Trump, Januari 20, 2017 wakati wa kukabidhiana madaraka mjini Washington. REUTERS/Carlos Barria/File Photo

Ikulu ya White House siku ya Jumapili, imeliomba Bunge la Congress la Marekani kuamua iwapo utawala wa Obama ulitumia vibaya "mamlaka yake ya uchunguzi" wakati wa kampeni za uchaguzi za mwishoni mwa mwaka 2016.

Matangazo ya kibiashara

Ombi hili linakujasiku moja baada ya shutma zilizotolewa na Donald Trump kwamba mtangulizi wake, Barack Obama aliagiza kufanya udukuzi wa mazungumzo ya simu ya Trump Tower , makao makuu ya kampeni ya aliye kuwa mgombea wa chama cha Republican mjini Washington katika uchaguzi wa urais. Trump hakuweka wazi shutma zake Jumamosi Machi 5.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sean Spicer, amesema Donald Trump na maafisa wa utawala wake hawatazungumzia chochote wakati ambapo Bunge la Congresslitakua bado halijafanya uchunguzi wake, na hivyo kuonyesha kuwa Bw Trump hajawa tayari kuweka wazi shutma zake dhidi ya Barack Obama.

"Habari hizi zilizohusu uchunguzi wenye lengo la kisiasa kabla tu ya uchaguzi wa mwaka 2016 zinasumbua sana," Sean Spicer amebainisha.

Donald Trump alimshtumu Barack Obama kuwa aliamuru maafisa wake wa usalama kufanya udukuzi wa mazungumzo ya makao yake ya kampeni mjini New York mwezi Oktoba katika wiki za mwisho za kampeni ya urais,huku akimwita mtangulizi wake kuwa ni " mtu maskini."

Msemaji wa Barack Obama haraka alikanusha shutma za udukuzi wa mazungumzo ya simu ya makao makuu ya kampeni za urais ya chama aliye kuwa mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump.