MAREKANI-TRUMP-OBAMA-HAKI

Mkurugenzi wa FBI afutilia mbali shutma za Trump dhidi ya Obama

Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Marekani la FBI James Comey amepinga madai ya Rais Donald Trump dhidi ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Barack Obama kwamba alidukua simu yake kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Marekani la FBI, James Comey, Januari 10, 2017.
Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Marekani la FBI, James Comey, Januari 10, 2017. REUTERS/Joshua Roberts/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari nchini Marekani viliwanukuu maafisa vikisema kuwa James Comey anaamini hakukuwa na ushahidi kuthibitisha madai ya Trump.

James Comey amesema kuwa amelitaka shirika la haki nchini humo kupinga madai hayo kwamba Obama aliagiza uchunguzi wa simu za Donald Trump wakati wa kampeni za uchaguzi uliofanyika mwaka jana.

Bw Comey anasema madai ya Donald Trump yanayoonyesha kuwa FBI ilivunja sheria kwa kudukua simu yake.

Madai ya Trump liripotiwa na gazeti la the New York Times na kuthibitishwa na NBC.
Idara ya haki haijatoa taarifa yoyote kuhusu ombi la James Comey.

Rais Donald Trump kutoka chama cha Republican kwa sasa anakabiliwa na uchunguzi mkali kuhusu uingiliaji wa Urusi ili kuunga mkono uchaguzi wake.

Mpaka sasa Donald Trump hajatoa ushahidi wowote kuunga mkono madai yake kwamba simu zake katika ofisi ya Trump Tower zilidukuliwa.