MAREKANI-WANAWAKE-JAMII-TRUMP

Donald Trump: Natoa heshima kubwa kwa wanawake

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye kabla ya kuchaguliwa kwake kuwa rais wa Marekani alitoa hotuba yenye utata kuhusu wanawake, na Jumanne wiki hii alitangaza kuwa anatoa heshima kubwa kwa wanawake, siku moja kabla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Jumatano Machi 8.

Wanawake wa DRC wakiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Machi 8, 2016.
Wanawake wa DRC wakiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Machi 8, 2016. Photo MONUSCO/Lassana Dabo
Matangazo ya kibiashara

"Ninatoa heshima kubwa kwa wanawake na kazi nyingi wanazozishikilia, ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya jamii yetu na uchumi wetu," Donald Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

"Kwa Siku ya Kimataifa ya Wanawake, unganeni nami kwa kutoa heshima kwa majukumu muhimu ya wanawake hapa nchini Marekani na duniani kote," Bw Trump aliongeza.

Katika video iliyotolewa mwezi Oktoba 2016 ambayo ilisababisha kashfa kubwa, Donald Trump alijigamba mwaka 2005 kuwa na uwezo wa kuwalipa wanawake anayewataka na "kuwafanya kile anachokitaka."

Matamshi hayo yalizua hali ya sintofahamu na maandamano makubwa nchini Marekani.

Mamilioni ya watu, hasa wanawake, waliandamana nchini Marekani siku moja baada ya Donald Trump kutawazwa, katika sehemu ya "Maandamano ya Wanawake" yaliyopangwa kwa kutetea haki za kiraia na dhidi ya rais wa Marekani Donald Trump, ambaye ni kutoka chama cha Republican.

Mashirika ya haki za wanawake pia yana hofu kuwekwa hatarini kwa haki ya utoaji mimba nchini Marekani, iliyohalalishwa mwaka 1973 na agizo la Mahakama Kuu "Roe V. Wade", baada Donald Trump kumteua Jaji mpya katika Mahakama Kuu, Neil Gorsuch.