UN-MAREKANI-TRUMP

Tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa yakosoa namna Trump anavyoongoza Marekani

Rais wa Marekani, Donald Trump.
Rais wa Marekani, Donald Trump. REUTERS/Jim Lo Scalzo/Pool

Mkuu wa tume ya haki za binadamu wa umoja wa Mataifa, amemshambulia rais wa Marekani, Donald Trump, akisema nchi hiyo ilihitaji kupata kiongozi bora ili kukabilia changamoto kama zile za ubaguzi wa rangi na dini.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake ya mwaka kwa baraza la usalama la umoja wa Mataifa, Zeid Al Hussein amesema kuwa "anaguswa na namna mtawala mpya wa Marekani anavyofanya mambo yake".

"Utawala bora na kiongozi bora alihitajika kuzungumzia masuala ya ubaguzi yanayoshuhudiwa, vurugu za kidini, kikabila na itikadi kali". aliongeza Zeid.

Zeid ameonya kuwa hatua ya Washington kuamua kutangaza vita ya waziwazi dhidi ya watu kutoka Mexico na Waislamu, pamoja na taarifa za uongo kuhusu unyanyasaji wanaofanyiwa wahamiaji, ni wazi yanachochea ubaguzi.

Akionesha wazi kumshambulia rais Trump, Zeid ameeleza masikitiko take kutokana na majaribio ya Trump kutaka kuwanyanyasa wanahabari na majaji wa mahakama.

Mashirika makubwa ya habari pamoja na makundi yanayotetea uhuru wa kutoa maoni, wanamtuhumu Trump kwa kuwanyanyasa waandishi jambo ambalo ni kinyume na maadili ya raia wa taifa kubwa kama Marekani.