MAREKANI

Marekani: Jaji aliyetoa zuio la kwanza akataa kutoa zuio jingine kupinga amri ya Trump

Moja ya bango linalosomeka amri mpya sheria ile ile.
Moja ya bango linalosomeka amri mpya sheria ile ile. REUTERS/Eric Thayer

Jaji wa mahakama moja nchini Marekani amekataa kutoa uamuzi wa dharura kuzuia ampri mpya ya rais Donald Trump, kuhusu wasafiri wanaoingia nchini humo kutoka kwenye mataifa sita aliyoyaainisha kwenye amri yake mpya.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umetolewa na jaji wa mahakama ya Seattle, james Robart, jaji yuleyule ambaye alitoa amri iliyofanya kazi na kuzuia utekelezwaji wa amri ya wali ya Trump kuhusu wahamiaji.

Jaji Robart amesema kuwenye uamuzi wake kuwa, mawakili walipaswa kuwasilisha nyaraka muhimu zaidi kwenye kesi hiyo.

Zuio jipya la siku 90 kwa raia kutoka kwenye mataifa 6 ya kiislamu kuingia nchini Marekani, linatarajiwa kuanza kutumika Alhamisi ya wiki ijayo, tayaro imeshaanza kupingwa pia kwenye majimbo kadhaa nchini humo.

Mawakili kwenye jimbo la Washington walimuomba jaji Robart aoanue wigo wa hukumu yake ya wali ili iendelee kufanya kazi pia kwenye agizo hili jipya la Trump.

Hata hivyo jaji huyo aliyoa sababu za kiutaratibu kuhusu shauri hili na kueleza ndio sababu iliyomfanya ashindwe kutoa uamuzi kuzuia amri mpya.

Jaji Robart anasema ili aweze kutoa uamuzi, ni lazima malalamiko yawasilishwe kwenye mahakama yake.

Wizara ya sheria imeshasema kuwa agizo la awali tayari lilishafutwa na kwamba uamuzi wa awali wa jaji hauwezi kufanya kazi kwenye amri ya pili. Kwa wale wanaopinga amri hii ya pili wanasema inafanana kabisa na ile ya awali.

Mafanikio waliyoyapata kwenye zuio la kwanza la mahakama, yalitokana na kueleza namna ambavyo makataa ya Trump ilikuwa kinyume cha katiba na ingeathiri biashara kwenye jimbo la Washington.

Msemaji wa ikulu ya Marekani, Sean Spicer, amesema utawala wake unaamini kuwa amri ya pili iliyotolewa na rais haina chembe ya utata wa kisheria kwa hivyo itatekelezeka.