Watu 38 wapoteza maisha katika ajali ya barabarani Haiti
Imechapishwa:
Watu 38 wamepoteza maisha nchini Hati na wengine 13 kujeruhiwa baada ya basi ndogo kugonga umati wa wanamuziki wa mitaani Jumapili katika wa Gonaives, kilomita 150 kaskazini magharibi mwa mji wa Port-au-Prince.
Baada ya ajali hiyo dereva wa basi aliamua kutimka kwa kuhofia kuuawa na wakaazi.
"Kwanza bus hilo liligonga wapita njia wawili, na kuua mmoja na kujeruhi mwingine," Marie-Alta Jean Baptiste, mkurugenzi wa kikosi cha ulinzi wa umma nchini Hati ameliambia shirika la habari la AFP. "Kisha dereva wa basi hilo aliondoka hapo kwa kasi na kujikuta amegonga bendi ya wanamuziki wa mitaani (Rara). Dereva huyo aliwakanyaga na watu 33 walifariki papo hapo."
Familia za wahanga hao bado zina hasira, huku wakiomba sheria ufuate mkodo wake na dereva huyo ahukumiwe kwa mujibu wa sheria.
Nchini Haiti, kutokana na hofu yakupigwa mawe hadi kufua na wakazi maeneo mbalimbali, madereva wanaofanya ajali kama hizo huamua kukimbia eneo la ajali.
Polisi iliingilia kati ili kuzuia hasira ya makundi ya watu ambayo yalitaka kulipiza kisasi.