MAREKANI-YAHOO-USALAMA

Udukuzi dhidi ya Yahoo: Watu wanne wakamatwa Marekani

Nembo ya Yahoo ! mjini Sunnyvale, California.
Nembo ya Yahoo ! mjini Sunnyvale, California. AFP

Serikali ya Marekani imetangza Jumatano wiki hii kwamba imewakamata watu wanne, ikiwa ni pamoja na maafisa wawili wa Idara ya ujasusi ya Urusi (FSB) kwa kufanya udukuzi mkubwa uliogunduliwa mwaka jana dhidi ya kampuni ya mtandao wa Yahoo.

Matangazo ya kibiashara

Udukuzi ambao ulianza mwaka 2014, unachukuliwa kama moja ya tukio kubwa zaidi kuwahi kufanywa duniani, ikiwa ni pamoja na "akaunti angalau milioni 500" zilizoharibiwa, wizara ya sheria ya Marekani (DOJ) imesema.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya sheria ya Marekani, maafisa wa upelelezi wa Urusi, Dmitry Dokouchaïev na Igor Souchtchine, "walilinda, walisimamia, waliwezesha na kulipa maharamia wa mitandao kukusanya taarifa kupitia mtandao Yahoo nchini Marekani na kwingineko."

Wawili kati yamaharamia hao wa mitandao ni miongoni mwa watu waliokamatwa Jumanne: wiki hii. Watu hao ni pamoja na Alexei Belan ( "Magg") kutoka Urusi, ambaye alikuwa tayari katika orodha ya wahalifu wengi wa intaneti wanaotafutwa na Marekani baada ya kutiwa hatiani kwa makosa yanayofanana kama hayo mwaka 2012 na 2013, na Baratov Karim, ambaye ni raia wa Canada mwenye asili ya Kazakhistan, na alikamatwa Jumanne wiki hii nchini Canada.

Baada ya kuingia katika mifumo ya mtandao wa Yahoo!, maharamia hao wa mitandao waliiba habari kutoka akaunti za watumiaji zaidi ya milioni 500, na pia walitumia baadhi ya taarifa zilizokusanywa kwa kupenyeza akaunti kwenye huduma nyingine zilizokua hewani kama vile Google, wizara ya sheri ya Marekani (DOJ) imesema.