MAREKANI-UJERUMANI

Trump na Merkel wakutana kuzungumzia Usalama

Raisi wa marekani Donald Trump na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,katika mkutano 17 mars 2017.
Raisi wa marekani Donald Trump na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,katika mkutano 17 mars 2017. REUTERS/Jim Bourg

Raisi wa Marekani Donald Trump amemkaribisha Kansela wa Ujerumani Angela Merkel katika ikulu ya white house kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wenye misimamo tofauti wanakutana na kufanya mazungumzo kwa mara ya kwanza tangu Trump kuingia madarakani.

Miongoni mwa agenda zinazotajwa kupewa kipaumbele katika mazungumzo ya viongozi hao ni pamoja na mapambano dhidi ya kundi la kijihadi la islamic state,kuimarisha jeshi la NATO na utatuzi wa mzozo wa Ukraine na Urusi.

Katika mkutano na waandishi wa habari Merkel amesema imekuwa jambo zuri kukutana na kuzungumza ana kwa ana na sio kuzungumziana.